Dkt. Kitila iwezeshe TRA kuwa na mifumo yote ya kidigitali badala kusumbua wafanyabiashara na ni lini wafanyabiashara ndogo watakuwa na maeneo yao?

Dkt. Kitila iwezeshe TRA kuwa na mifumo yote ya kidigitali badala kusumbua wafanyabiashara na ni lini wafanyabiashara ndogo watakuwa na maeneo yao?

Richard

JF-Expert Member
Joined
Oct 23, 2006
Posts
15,692
Reaction score
23,038
Moja kwa moja kwenye mada ambapo leo hii nimekusikia ukitoa tamko kwamba sasa TRA itaja na mfumo bora wa nyaraka wa kukusanya kodi kuanzia Julai 1, 2024.

Tatizo lililopo TRA ni upigaji ambapo maofisa wa TRA hujidamka mapema asubuhi kuwahi kusumbua wafanyabiashara na kugeuza usumbufu huo kuwa ni kero.

TRA haiwezi kukwepa "office automation" ambapo mifumo yake ya kutumia karatasi yabidi kubadilishwa iwe ya kidijitali , jambo linoweza kuisaidia TRA na serikali kuongeza mapato.

Ikiwezekana TRA yaweza kununua software ambazo ni za kisasa zaidi kutoka nje ya nchi ambazo zaweza kubadilisha kabisa mfumo wa kukusanya kodi khasa kwa wafanyabiashara. Kugeuza mifumo ya TRA kuwa ya kidigitali zaidi kutawezesha kuokoa muda, kuondoa makosa madogomadogo yaani errors, kuchanganyua data au data analysis na kuwezesha kupanga mipango sahihi ya kodi.

Huko mbele tuendako mfumo wa kodi ni lazima utakuwa ukizingatia zaidi "Data" ambapo ni lazima wafanyabiashara wote wasajiliwe na wajulikane. Utaratibu wa kuwasajili wafanyabiashara, wajasiliamali na wachuuzi wengine wa kutoka China ni lazima wawe na TIN na watambulike.

Kubadilisha mfumo wa kodi si tu kuhakikisha walipa kodi wafanya hivyo (compliance) lakini pia kwatoa mwanya kuwasaidia maofisa wa TRA kukusanya kodi kwa njia sahihi na za kisasa zaidi na kupata matokeo mazuri na yaso na dosari au twaita accuracy and efficiency gains.

Suala la utitiri wa kodi nalo ni la kuliangalia si tu kuleta kodi mpya kila mtu akiamka asubuhi aja na kodi au tozo. Kwa mfano wachuuzi ambao hawana visimba wawe na kodi yao tofauti na wale wenye visimba sambamba na akina mama ntilie na wauza maji ya matunda, nguo, mitumba na kadhalika.

Wafanya biashara wenye maduka wawe na kodi yao na hawa kuwa hutozwa pia kodi ya majengo au kiwanja au vinginevyo ni lazima wawe na njia sahihi ya kulipa kodi zao. Serikali yaweza kukusanya hizi kodi bila shurti kutoka kwa wafanyabiashara endapo yatumia njia sahihi, bora na zisizowasumbua hawa watu maana wao pia ni binadamu na wastahiki heshima.

TRA ni chombo kikubwa kilichoko nchi nzima na yenye chuo chake cha kodi ambacho hufunza maofisa wa kodi. Hivyo ni lazima TRA waangalie madhara ya kusababisha migomo kama mgomo uliopo sasa wa wafanyabishara. Kwanza mgomo hubababisha upotevu wa mapato kwa wafanyabiashara wenyewe na TRA. Pili migomo hii huatarisha kuwepo na uvunjifu wa amani hivyo busara yahitajika katika kushughulikia matatizo ya wafanyabiashara yanosababiswana TRA.

Mwisho but last, maeneo ya Kariakoo yamejaa sana wafanyabiashara na uwingi wao ni hatari kiafya, kimazingira na kiusalama. Tunao hata ndugu zetu wachina nao ni wachuuzi wa bidhaa hizohizo ambao watanzania nao waziuza maeneo hayo. Maoni yangu ni kwamba hawa wachina mfumo wa kodi uwe wawatoza tofauti na watanzania ili kuwasumbua (discourage) kuwafanya wapunguze kuingiza nchini bidhaa zilozo chini ya viwango na hatari kwa matumizi ya binadamu.

Pia ni jambo la uzuri endapo utafikiria kuanzisha maeneo mapya ya wafanya biashara ambayo yana visimba, umeme, vyoo na mazingira mazuri ambapo wale wafanyabishara wenye uwezo waweze kuhamia kule ili kupunguza msongamano uliopo mitaa ya Kariakoo jambo ambalo litawezesha pia serikali na TRA kupata mapato sahihi kutoka kwa wafanyabiashara hawa.

Hili la kuwatafutia wafanyabiashara wadogo waso na maduka haliwezi kuwa ni tatizo kubwa endapo serikali yatafuta maeneo na kuwasaidia hawa ambao wengi wao ni wahitimu wa hadi vyuo vikuu ambao hawawezi kutoelewa sera ya serikali ya kuwatafutia maeneo maalum.

Mheshimiwa waziri wewe ulikuwa hapa JF ukitoa maoni yako lukuki kuhusu namna ya kurekebisha siasa, uwajibikaji wa serikali na wanasiasa. Naona bado hatujafikia huko na litakuwa ni jambo la kuleta imani kuona unatumia uwezo wako na nafasi yako ukiwa waziri wa uwekezaji kuhakikisha TRA yafanya kazi zake sawa na malengo ya kuundwa kwake.
 
Very true. Watu wengi hawalipi kodi. Na mifumo iliyopo imeshindwa kufanya hivyo. Jambo hili hufanya serikali kuwaumiza watoa kodi wachache inaowajua.
Mfumo huu uliopo sasa unaweza kuchochea rushwa ambayo mwishowe huzaa migomo kama huu wa sasa.

Pia utatuzi wa migogoro uwe na uwezo wa kutoa suluhu ya kudumu. Haiwezekani leo Waziri mkuu akubaliane na wafanyabiashara, halafu kesho yake akatokea Waziri au Kamishena akaja kivingine. Na hili ndo lililotokea Kariakoo

Pia tupunguze kuwafanya walipa kodi mtaji wa kisiasa. Yawezekana wakati Serikali inapita huku, "chama" nacho kinapita upande mwingine kulinda "wapiga kura" wake. Sasa kwa sababu watendaji ni wale wale kwenye "chama" na Serikali, lazima kutakuwa na mkanganyiko.
 
HAKUNA MWANADAMU ANAYEPENDA KULIPA KODI HAPA DUNIANI AWE MZUNGU, MUHINDI AU MUHARABU, ISPOKUWA KINACHOSABABISHA WATU KULIPA KODI KWA NYAKATI HIZI NI MFUMO BORA UNAOLAZIMISHA MTU KULIPA KODI KWA LAZIMA, INDIRECT TAXATIONS,
°mfumo, mfumo, mfumo.
 
Kinachonisikitisha ukifika TRA kwaajili ya kukadiriwa, afisa anahesabu zake kichwani, hata umwambie vipi kuhusu mapato unayopata katika biashara yako kabla ya kodi, afisa mkadiriaji hakuamini asilani abadani atakukadiria kodi isiyo rafiki mpaka unajiuliza...hivi huyu afisaa uzoefu ameupata wapi kufanaisha kodi ya mwenye duka la vifaa vya ujenzi ifanane na muuza duka la dawa za asili... kwanini kodi ya duka la kubadilisha fedha za kigeni ipo chini kuliko mwenye kuuza viatu..
 
Kinachonisikitisha ukifika TRA kwaajili ya kukadiriwa, afisa anahesabu zake kichwani, hata umwambie vipi kuhusu mapato unayopata katika biashara yako kabla ya kodi, afisa mkadiriaji hakuamini asilani abadani atakukadiria kodi isiyo rafiki mpaka unajiuliza...hivi huyu afisaa uzoefu ameupata wapi kufanaisha kodi ya mwenye duka la vifaa vya ujenzi ifanane na muuza duka la dawa za asili... kwanini kodi ya duka la kubadilisha fedha za kigeni ipo chini kuliko mwenye kuuza viatu..
TRA ikiwa na mfumo sahihi wa kodi yaweza kabisa kutofautisha aina za wafanyabiashara. Hii yaweza kufanywa katika hatua ya awali ya kumsajili mfanyabiashara ambayo itataka TIN, aina ya biashara eneo la biashara na mapato yake kwa mwaka.

Suala la kufikiria kodi bila kuwepo mfumo sahihi na imara au Robust Tax System, kwatengeneza mianya ya upigaji na ufisadi.
 
Naunga mkono hoja
Hivi hatuwezi kugroup kuanzia wajasiamali wadogo mpaka wakubwa au wafanyabiashara wadogo mpaka wakubwa kulingana na mitaji yao na kuwa na aina moja ya kodi katika group husika , kwamba mtu akiamua amka hasubui na kuanzisha biashara ya kuanzia mtaji flani anajua automatically anatakiwa kulipa kodi ya sh ngapi,

Mjasiliamali akitaka kuanza ujasiliamali wa mtaji flani anajua direct kwa mwaka fungu lake la kodi sh ngapi na mwongozo ikawa wazi ,ila ikawapo fain kali kwa yule anaekutwa amedanganya mtaji wake inapobainika, lakini pia pakawapo form kwa mfanyabiashara kuupdate mtaji wake kila mwaka ili kumwezesha ama kuendelea na kodi ya awali , au kuongeza au kupungua kulingana na mtaji wake wa mwaka husika?

Mfano
Tukasema

Mtaji kuanzia elfu 10 -50 kodi kwa mwaka ni elfu 20 ,kwamba endapo wewe ni mfanyabiasha au mjasiriamali wa mtaji huo basi kwa mwaka utalipa elfu 20 , ila maushuru mengine ya kijinga lazima yaondoke.

Binafsi hii watu wakituliza vichwa na kuja na mfumo ulioboreshwa kupita wazo hili TRA inaweza kukusanya kodi nyingi na watu kufanya biashara kwa amani, na hii inaweza mwezesha TRA kuwa na wakala wake kila kijiji au mtaa ambae anakuwepo kwa ajili ya kufuatilia watu wake katika mtaa wake kwa mwaka mzima kama wamelipa ,na kama watu wake wapo na changamoto na kuziwasilisha mamlaka za TRA wilaya .

Pia hii inaweza saida kuondoa rushwa ,kuvuja kwa mapato, viburi na kutojari wa baadhi ya wafanyakazi ndani ya TRA,
Tusichojua mapato mengi yanapotezwa kwenye ukadiriaji wa kodi , kwamba mnaweza kuwa watu mnafanya biashara moja mtaji mmoja ila makadirio ya kodi yako tofauti.

Leo ukitaka kufanya mwamala wa pesa unajua kabisa kwamba ml tano mtandao flani nakatwa sh flani ,iwe hivyo hata kwenye kodi za biashara kwamba kwa mtaji wangu sh flani nitalipa kodi kwa mwaka sh flani basi.
 
Back
Top Bottom