mbingunikwetu
JF-Expert Member
- Feb 17, 2015
- 13,897
- 18,477
Inabidi tuseme wazi bila kupepesa macho!! Tatizo la Dr Koboko ni kuwa anaona kula kwa kadri ya urefu wa kamba ya udaktari tu haitoshi! anataka aunganishe na ile ya ufamasia!! Sababu yake ni kuwa eti kwa sababu anaweza kutoa dawa pharmacy bila mgonjwa kuwa na prescription
Hataki mfamasia atoe dawa kwa mgonjwa!! Si kwa kuwa mfamasia hawezi kutoa dawa kwa mujibu wa prescription (kwa dawa zinazohitaji prescription), eti kwa sababu mfamasia hayajui magonjwa!!
Mfamasia hahitaji ayajue magonjwa (japo anayajua kwa kiasi fulani) ili aweze kutoa dawa!! Siyo jukumu la mfamasia kujua magonjwa, maana hiyo ni kazi ya daktari!!
Kutokujua magonjwa hakumfanyi ashindwe majukumu yake ya msingi kwenye pharmacy!
Dr Koboko anataka Daktari ndiye atoe dawa pale pharmacy na hakuna sababu ya mgonjwa kwenda na cheti maana Daktari anayajua magonjwa!! Kwa hiyo Dr Koboko anataka kutumia pharmacy kama dispensary pia au clinic!!
Hawa ndio madaktari wetu halafu analisema hilo hadharani bila aibu!! Anauliza, je mgonjwa akienda pharmacy bila cheti cha Daktari huyo mfamasia atamsaidiaje? Kwake hiyo ni hoja yenye nguvu!! Jibu ni kwamba mgonjwa akienda pharmacy kutibiwa ataambiwa kuwa pharmacy sio hospitali!! Atashauriwa aende kwa hospitali kama hitaji lake linahitaji dawa zinazotolewa kwa prescription ya daktari.
Wafamasia wote wanajua hivyo, na kama mmoja akikiuka atashughulikiwa na bodi ya pharmacy kwa mujibu wa sheria!! Nanukuu mawazo ya Dr Koboko:
"✓Kazi ya Mfamasia ni kutunza na kuhifadhi dawa, kusambaza maeneo yenye uhitaji pamoja na kutengeneza dawa viwandani na siyo kutoa dawa moja kwa moja kwa mgonjwa . Kwa hiyo kazi yake siyo drugs Administration, hii ni kazi ya watu wengine. Mfamasia hajasomea Magonjwa wala wadudu wanaosababisha maradhi, hajasomea dalili za magonjwa.
Hivi anapoenda mgonjwa kwenye duka la dawa na hana cheti cha daktari, Mfamasia anajua Diagnosis ya ugonjwa wake? Amesomea dalili? Ni maduka mangapi yanayotoa dawa kwa vyeti vya madaktari nchini? Hivi mnajua kuwa mnataka kuliangamiza taifa kwa maslahi ya wachache?"
Unaona, Koboko hataki mfamasia atoe dawa moja kwa moja kwa mgonjwa wakati pale pharmacy ndiyo kazi ya mfamasia kutoa dawa kwa mgonjwa!! Kwa maneno mengine pharmacy au duka la dawa halihitaji kuwa na mfamasia! Eti atafanyaje kama mgonjwa ataenda pharmacy bila cheti cha daktari!! Jibu ni kuwa haitakiwi mgonjwa aende pharmacy bila cheti cha daktari kama dawa anayohitaji inatakiwa kuwa na prescriptrion!! Jibu siyo kuruhusu mgonjwa aende pharmacy bila cheti cha daktari kwa sababu eti atamkuta daktari hapo!!
PHARMACY SIYO MAHALI PA TIBA!! KWA HIYO DAKTARI HATAKIWI HAPO!! DAKTARI AKITAKA KUTIBU AENDE HOSPITALINI NA SIYO PHARMACY!! NA MGONJWA AKITAKA KUTIBIWA AENDE HOSPITALINI NA SIYO PHARMACY!!
Dr Koboko anataka ku-practice profession yake pharmacy!! Dr Koboko hajui mahali sahihi pa ku-practice!! ni maajabu!! Halafu anataka wafamasia watoke pharmacy waende viwandani!! na wawe mastoo keeper tu wa dawa!!
Ushauri kwa Dr. Koboko: Ukitaka kuunganisha kamba ya udaktari na ufamasia ili uongeze eneo la kula NENDA KASOMEE KOZI YA PHARMACY PIA MIAKA 4 + MWAKA 1 WA INTERN kisha nenda kafungue pharmacy na utibu kinyemela maana pharmacy siyo eneo muafaka la kufanyia tiba!