Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli, CCM na wananchi dhidi ya Lissu, CHADEMA na wazungu

Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli, CCM na wananchi dhidi ya Lissu, CHADEMA na wazungu

Wakudadavuwa

JF-Expert Member
Joined
Feb 17, 2016
Posts
17,506
Reaction score
16,003
Ndugu zangu,

Kwa mujibu wa aliyewahi kuwa Rais wa Marekani marehemu Abraham Lincoln anasema "Demokrasia ni serikali ya watu, iliyowekwa na watu kwa ajili ya watu"

Huku Magufuli na chama chake CCM wakionekana kujifungamanisha na Watanzania ili kupata uhalali wa kuwaongoza.

Kwa upande mwingine, Tundu na chama chake cha Chadema wamejikita kupata ushawishi kutoka kwa wa akina Amsterdam, kuhutubia Wakenya.

Mjadala hapa kwa kuzingatia maana ya demokrasia kama ilivyotafsiriwa na Lyncoln utagundua kwa uwazi kuwa kati ya Magufuli na Tundu ni nani anawakilisha serikali ya Watanzania na nani anawasilisha serikali ya wasio Watanzania.

Tujadili kwa utulivu.
 
Mwisho wenu umewadia! Hamtaamini macho yenu kwa mnachokitengeneza mwaka huu!

Kwa hiyo Magufuli anaejifunganisha na watanzania ndo yeye na tume yake na vyombo vyake wanawaengua wagombea wa upinzani, kuwateka na kuwabambikia makesi wapinzani ili wasishiriki uchaguzi eeh?
 
Mwisho wenu umewadia! Hamtaamini macho yenu kwa mnachokitengeneza mwaka huu!

Kwa hiyo Magufuli anaejifunganisha na watanzania ndo yeye na tume yake na vyombo vyake wanawaengua wagombea wa upinzani , kuwateka na kuwabambikia makesi wapinzani ili wasishiriki uchaguzi eeh?
Serikali ya wananchi haiwezi kuogopa demokrasia Wala upinzani wa mtu mmoja,Wala kulazimisha kupita Bila kupingwa.TAFAKARI
 
Mwisho wenu umewadia!!! Hamtaamini macho yenu kwa mnachokitengeneza mwaka huu!!!

Kwa hiyo Magufuli anaejifunganisha na watanzania ndo yeye na tume yake na vyombo vyake wanawaengua wagombea wa upinzani , kuwateka na kuwabambikia makesi wapinzani ili wasishiriki uchaguzi eeh???
Kamanda soma uelewe hoja, acha papara.
 
Back
Top Bottom