Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli gwiji la lilitokomeza virusi vya Corona na kuushangaza ulimwengu; Oktoba 28 anastahili ushindi wa kishindo

Alex Fredrick

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2016
Posts
697
Reaction score
1,358
Mwishoni wa mwaka jana Dunia iliingia kiwewe baada ya kuripotiwa ugonjwa wa virus vya Corona huko Mji wa Wuhan Nchini China

Badae maambukizi yakaenea kwa kasi Ulaya hasa Italy na nchi jirani kama Spain, Ufaransa nk

Hatimaye Marekani, Brazil, Urusi na India ndo wamekuwa virana wa maambukizi ya virus vya corona sasa.

Marekani pamoja na Rais Donald Trump kufanya mambo makubwa ndani ya miaka yake minne tu lakini swala la kuzembea kuchukua tahadhari dhidi ya virusi vya Corona linatishia kuweza kurudi tena kama Rais kwenye ngwe yake ya pili

Barani Africa virusi vilivyoingia tu Nchini Tanzania kupitia Rais wetu Dr John Pombe Magufuli akaja na maazimio mawili ambayo Dunia nzima haikumuelewa.

Pale aliposema Tufunge kama Taifa kwaajili ya maombi kwa Mungu na pili kuhoji ofisi ya maabara ya Taifa jinsi gani wanavyopima sampuli vya virus vya Corona.

Dunia ilitucheka sana na majirani zetu wakatubeza kiasi kwamba Gazeti moja nchini Kenya lilisema Magufuli ni "Kichaa na kina Bill Gates wakatabiri kwamba Africa muda mrefu maiti zitakuwa zinaanguka barabarani.

Kamanda wa vita na Jemedari Mkuu Kilongora Dr John Pombe Magufuli akaziba Masikio na kutoa tamko kwamba hii ni vita kwahiyo kila mtu apambane kivyake

Hatimaye chini ya Dr John Pombe Magufuli tuliishinda Covid 19 kwa 100% ndani ya muda mfupi sana na Dunia kuanza kutushangaa imekuwaje Rais Magufuli ameiishinda Covid 19

Rais wetu Dr John Pombe Magufuli amefanya mambo makubwa mno ndani ya miaka mitano kiasi kwamba sina mashaka na kushinda tena tarehe 28 October 2020

Lakini hili ya virusi vya Corona limeonyesha Tanzania tuna kiongozi mahiri,jasiri na zaidi mwenye maamuzi magumu kwa ustawi wa Taifa letu

Shime wa Tanzania wote tarehe 28 October 2020 kwa pamoja wale wote ambao tumejiandikisha tuende kwa ari kubwa kumpa kura za ndio mgombea kupitia Chama cha mapinduzi Dr John Pombe Magufuli

Week ijayo ntaeleza sababu zingine lukuki ambazo zinamfanya Dr John Pombe Magufuli kuendelea kuongoza Taifa hili miaka mingi ijayo zaidi ntajika kwa mambo ya maendeleo ndani ya miaka mitano iliyopita

YABISO CANIDAA?

CANDINDAA DR JOHN POMBE MAGUFULI OCTOBER 28 2020

Alex Fredrick
Dar es salaam Tanzania



 
Ukoina mtu anaandika hivi ujue huyu ni Lumpen!
 
Pia usisahau na ugwiji wake wa kupoteza watu kiholela, kupenda wanawake waupe na woga wake wa kumuogopa Lissu.
 
Magufuli huyuhuyu aliyeenda kujificha chatoo wakati korona inashambulia nchi?!.

acheni utani nyie korona imelionea "huruma" bara lote la afrika kwa ujumla na sio tz pekee tu.
 
mbinu za kutumia wasanii, kupiga magoti, kulia na kutishia wananchi ambao hawatamchagua kaona hazilipi... sasa hivi yupo bize huko Twitter kuomba kura lakini huko nako kakutana na kina Kigogo & co wanampa za uso kama zote.

ukisikia maji kushingo ndiyo hii sasa!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…