Uchaguzi 2020 Dkt. Magufuli: Jina Langu Lipo Namba Moja, Usihangaike Kuangalia Kwingine

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,880
Reaction score
6,368
Mgombea Urais wa JMT kupitia CCM, Dkt. John Magufuli amesema jina lake na la Mama Samia lipo juu katika karatasi za kupigia kura hivyo wananchi wasihangaike kuangalia kwingine



Amesema, "Wewe angalia juu utalikuta jina la John Pombe Joseph Magufuli, utalikuta la Mama Samia Suhulu, utakuta na box la kuweka 'tick'. Wewe weka 'tick' kunja karatasi lako, dumbukiza kwenye box nenda ukampumzike nyumbani"

Katika mkutano wa kampeni uliofanyika Korogwe Mkoani Tanga, Dkt. Magufuli amewaambia wananchi wasihangaike kuangalia kwengine kwasababu wale hawawahusu

Amewaelekza wananchi kuwa, wakati wa Uchaguzi ni wakati wa kuamua kama wanataka maendeleo au 'blah blah'
 
JPM keshashinda leo kaomba "connection" ya wabunge na madiwani. Hakika anastahili mafiga matatu ili Amsterdam na vibaraka wake wachanganyikiwe
 
Hahahh
Kushoto kulia, kushoto kulia
Wapo wanaopinga jitihada zako
Wanaona Aibu wanaogopa, wanaogopa

Sina Chama Lakini Nampa MAGUFULI
Siwezi kumpa Mtu kula akaweke rehani Madini Yetu [emoji16][emoji16][emoji16]
 
Karatasi ya kura ili iwe fair ilitakiwa ziwe randomly printed, yaani karatasi hii chama flani kipo juu, karatasi nyingine chama kingine kipo juu, completely random. Kuweka mtu moja juu ukimpa bibi kachoka anafungua karatasi anaweka tiki moja anaondoka unahisi ataweka chini kabisa au juu?
 
CCM hawana nia njema na wapiga kura
 
Hahahh
Kushoto kulia, kushoto kulia
Wapo wanaopinga jitihada zako
Wanaona Aibu wanaogopa, wanaogopa

Sina Chama Lakini Nampa MAGUFULI
Siwezi kumpa Mtu kula akaweke rehani Madini Yetu [emoji16][emoji16][emoji16]
Mimi ni mtumishi wa umma. Kura yangu siwezi kuipeleka kwa kiongozi dhalimu aliyenitesa kwa miaka mitano.

Nasema hadharani kwamba nitamchagua Tundu Lissu kwa maendeleo ya kweli.

Huyo dikteta akalime nyanya chungu huko Geita.
 
Ni jambo jema!
 
Haina tatizo, kokote watakapo elekezea kichwa, tunachinja tu! Wabibi na wababu hao wanaotegemewa ni asilimia chache tu ya wapiga kura! Ni vizuri pia CCM nao wakaokota kura chache hapa na pale, lakini Rais ni Lissu!
 
Huyo Bibi Atakae Mpigia kura Tundu Lissu Nani mkuu?
Ninyi wengi Mnamjua Tundu Lissu ikiwemo na hawa watu Robert Amsterdam, Jeffrey Smith, Pompoe, Maria Salungi Nk Ndio Maana mnaweza kumuelezea vizuri Tundu Lissu.

Watu wa Vijijini hawamjui Tundu Lissu wanamsikia sikia tuu juu juu
Lakini ukisema MAKUFULI hakuna asie Mjua Mzee [emoji16][emoji16][emoji16]
 
#JPM is the best president ever [emoji110]
 
NEC wametumia akili sana juu mpangilio wa wagombea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…