Filosofia ya Rorya
JF-Expert Member
- Sep 20, 2021
- 3,211
- 3,611
Kwa spidi ya kazi ya Mhe. Rais wa SMZ Dr. Hussein Ali Mwinyi, ni wazi kwamba maneno ya Mhe. Magufuli kwamba ninataka kuibadili Zanzibar hayakumaanisha kwamba atawapa Wazanzibari fedha bali kumbe sasa imedhihiri kwamba alimaanisha atawapa kiongozi mahiri wa mfano atayeibadili Zanzibar kwa muda mfupi kama Mhe. Abeid Amani Karume na kama Mhe. Magufuli walivyofanya, spidi hii ya kazi ndani ya awamu moja tu pia rekodi yake duniani iliandikwa na Mhe. Joseph Stalin na Mhe. William Shadrack Tubman 1944 - 1971 (rais wa 19 wa Liberia).
Ndani ya mwaka mmoja wa kazi ya mfano, Mhe. Dr. Mwinyi ameishakuza uchumi wa visiwa hivyo vya karafuu, mwani na vanilla kwa asilimia 8.8 (Prof. Luoga) ikiongoza EAC ndani ya janga la dunia la Corona, ni katika mwendo huo huo Mhe. Magufuli aliingiza JMT kwenye uchumi wa pato la kati ndani ya dunia kuchanganyikiwa na janga hilo hilo la Corona.
Mhe. William Shadrack Tubman aliwaunganisha wananchi wake waliogawanyika makundi mawili ya Waliberia wazawa (Afro-Liberians) na Waliberia wenye asili ya Marekani (Americo-Liberians), Tubman mwaka 1950 aliifanya Liberia kuwa ya pili duniani kwa kasi ya ukuaji uchumi na ya pili duniani kwa kuzalisha chuma-cha-pua ikitanguliwa na Ujerumani na ya kwanza duniani kwa kuzalisha zao la mpira, alivutia uwekezaji wa jumla ya thamani ya US $ 1 bl (takriban Tzs. 2.2 tr kwa sasa). Amepewa heshima kama Baba wa Liberia mpya.
Mhe. Rais Franklin Delano Roosevelt wa Amerika almaarufu kama FDR, picha/taswira ya Amerika ya leo inayomiliki asilima 14 ya pato la dunia nzima ikiwa na pato la takriban dola za Marekani 30 tr kwa mwaka; aliiona mwaka 1933 alipokuwa akitengeneza Dira (mpango mkakati wa kufufua uchumi kufuatia anguko la uchumi “Great Depression 1929-1939”), katika hotuba yake ya kuapishwa kuwa rais wa 32 alisema “the only thing we have to fear is fear itself” “kitu pekee tunachohitaji kuhofia ni hofu yenyewe” Rais FDR aligundua ukubwa wa tatizo la ajira lililofikia kati ya asilimia 80 na 90 katika baadhi ya majimbo na hivyo watu 15 ml wakakosa ajira baada ya baadhi ya mitaji iliyowekezwa kufilisika, watu wakawa wanatoa amana zao kwa kasi kubwa, ndipo akatangaza likizo-ya-kibenki ya siku 4 ili watu washindwe kuhamisha amana zao toka mabenki.
Baraza la Congress likapitisha sheria ya Roosevelt ya dharura ya kibenki (Roosevelt Emergency Banking Act); ambayo ilisanifu upya mabenki na kufunga zile ambazo zilifilisika, siku tatu baadaye FDR akawaomba Wamarekani kurudisha amana zao benki ambapo hadi mwisho wa mwezi huo takriban robo tatu ya mabenki yalirudi sokoni. Huu ni mkakati mojawapo kati ya mingi aliyotekeleza kufufua uchumi wa Amerika zikiwemo kilimo, viwanda na biashara. Mhe. Rais Dkt. Magufuli anaakisika kwenye modeli hii ya FDR kwa jitihada zake makini za kuratibu mageuzi ya kiuchumi akigusa sekta muhimu za taasisi za fedha, madini, nishati, miundombinu, kilimo, viwanda na biashara zikiwemo biashara ndogondogo na za kati ambazo ndizo zina walipa kodi wengi zaidi.
Dunia inayo ya kujifunza toka Zanzibar, leo Zanzibar imeondolewa kwenye orodha ya maeneo yenye Malaria kwenye sayari ya dunia. ZANZIBAR NI MALARIA FREE ZONE.
Mhe. Magufuli anaishi kama wanavyoishi Joseph Stalin, William Tubman, Abeid Karume, Mwl. Nyerere, Nelson Madela, Mao Tse Tung na FDR nikitaja kwa uchache. Ni vivyo hivyo Dr. Hussein Ali Mwinyi (kama atahakikishiwa ushirikiano wa kutosha) ataendelea kuishi kwenye mtima wa dunia hata baada ya kustaafu.
...Mwinyi, nakupa huu ufunguo, ukaifungue Zanzibar kimaendeleo. Picha ya maktaba imetumika kufikisha tu ujumbe japo kihalisia hapa Dr. Mwinyi alikuwa Waziri wa Ulinzi.
Taswira kwa hisani ya google.