jingalao
JF-Expert Member
- Oct 12, 2011
- 36,197
- 29,717
Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mgombea urais kupitia CCM amesisitiza kuwa atastaafu rasmi Urais na kamwe hataongeza hata siku moja ifikapo 2025.
Kauli hii inaondoa kiwingu kilichokuwepo kuwa upo uwezekano wa kubadilishwa katiba ili aendelee kudumu kama walivyo marais wengi barani Afrika.
Tanzania imekuwa na utamaduni wa marais kuachia ngazi kila baada ya miaka 10 ya kuhudumu Ikulu.
My Take: Pamoja na kufanya Mengi bado Rais Magufuli ataiheshimu katiba na utamaduni wa nchi yetu.
NOTE: Kauli hii inarudiwa baada ya kauli nyingine kama hii > Rais Magufuli: Nitastaafu muda wangu ukiisha, sina mpango wa kuongeza hata dakika moja