Dkt. Mathuki akabidhiwa rasmi katibu mkuu EAC, Mfumukeko aagwa

Waziri2025

Senior Member
Joined
Sep 2, 2019
Posts
148
Reaction score
379
Katibu mkuu mpya wa jumuiya ya Afrika mashariki, Dkt Peter Mathuki ameahidi kuzitembelea nchi wanachama wa jumuiya hiyo ili kuibua Changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi na namna ya kuzipatia ufumbuzi.

Aidha amewataka wafanyakazi wa jumuiya hiyo kushikamana kwa pamoja na kutokubali kutumika kwa lengo la kudhorotesha maendeleo ya jumuiya hiyo ili wananchi waweze kupata maendeleo ya haraka.

Akiongea Jana katika hafla ya kukabidhiwa wadhifa huo iliyofanyika katika makao makuu ya EAC yaliyoenda sanjari na kumuaga mtangulizi wake ,Liberath Mufumukeko aliyemaliza muda wake wa miaka mitano.

Dkt Mathuki aliahidi kuitumikia nafasi hiyo kwa moyo wake wote ili kupambana na changamoto zinazowakabili wananchi wa kumuiya ya Afrika mashariki.

"Kila mwanajumuia ananafasi ya kuchangia maendeleo ya kumuiya hii, tuchape kazi ili kuwasaidia wanachi wetu wanaoteseka na Mimi nitaweka maisha yangu yote kuitumikia kumuiya ya Afrika mashariki"alisema

Dkt Mathuki kabla ya wadhifa huo aliwahi kuwa mwenyekiti wa Baraza la biashara la Afrika mashariki(EABC) na anakabiliwa na changamoto ya kurejesha mahusiano ya kibiashara kwa Baadhi ya nchi wanachana pamoja na kulegelega katika uchangiaji wa michango ya nchi nchi wanachana na kupelekea kwa Baadhi ya miradi kukwama.

Ends....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…