Dkt. Mpango aagiza Manispaa ya Tabora kumshughulikia mtumishi aliyefanya ubadhilifu hospitali

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610
Your browser is not able to display this video.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Philip Mpango, ameuagiza uongozi wa Manispaa ya Tabora kushirikiana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa, kuhakikisha wanamfikisha katika vyombo vya sheria aliyefanya ubadhirifu, wakati wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tabora.

Makamu wa Rais ametoa maagizo hayo baada ya kuweka jiwe la msingi ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Tabora Kata ya Mpela, Mtaa wa Uledi, inayogharimu shilingi bilioni 2.8.

Makamu wa Rais pia, amekemea tabia ya kukiuka taratibu za manunuzi na kuwataka watumishi wa umma, kuhakikisha wanazingatia sheria katika taaluma zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…