Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango amekabidhi mitungi ya gesi 650 iliyotolewa na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC), ikiwa ni uhamasishaji wa matumizi ya nishati safi nchini.
Dkt. Mpango ni mgeni rasmi katika kuhitimisha mkutano wa mafunzo wa 109 wa watayarishaji wa Vipindi vya Elimu kwa Umma (WASHITIRI) kupitia TBC, unaofanyika katika Ukumbi wa City Park Garden Jijini Mbeya.