Wizara ya Ardhi
Member
- May 14, 2024
- 94
- 75
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ameiagiza Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kushirikiana na uongozi wa Mkoa wa Dodoma kuhakikisha ardhi inayotengwa kwa ajili ya kilimo cha zabibu inalindwa na usifanyike ujenzi wa makazi katika ardhi hiyo.
Dkt. Mpango ametoa agizo hilo wakati wa uwekaji Jiwe la Msingi la Kiwanda cha Kusindika Zabibu kilichopo katika eneo la Chinangali wilayani Chamwino mkoani Dodoma ikiwa ni siku yake ya kwanza ya ziara ya kikazi mkoani humo.
“ Waziri wa Ardhi na Mbunge wa Jimbo hili la Chamwino ( Deogratius Ndejembi) yupo hapa, naelekeza ukae na wataalam wa wizara ya ardhi na wale wa mkoani ili wahakikishe ardhi ambayo imetengwa kwa ajili ya kilimo cha zabibu inasimamiwa kikamilifu na ujenzi wowote wa makazi usifanyike na maeneo yote yaliyotengwa kwa ajili ya kilimo hicho yanabaki kama yalivyopangwa,” Amesema Mhe Makamu wa Rais.