Dkt. Mpango: Kuna Mawakili wanatuhumiwa kuchukua rushwa. Profesa Hoseah: Wimbi la Polisi na Vyombo vya Dola kukamata Mawakili ovyo limetulia

Dkt. Mpango: Kuna Mawakili wanatuhumiwa kuchukua rushwa. Profesa Hoseah: Wimbi la Polisi na Vyombo vya Dola kukamata Mawakili ovyo limetulia

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760

Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili Tanganyika (The Tanganyika Law Society - TLS) unafanyika Jijini Arusha, leo Mei 11, 2023 ambao Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango ndiye mgeni rasmi katika shughuli hiyo.​


RC Mongella anatoa neno
Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella amepata nafasi ya kutoa neno baada ya mgeni rasmi na washiriki wote kuwasili.

Mongella amesema: Rais ameeleza tuwapatie ardhi Chama cha Wanasheria wa Afrika Mashariki ardhi, tumelitekeleza hilo.

Serikali ya Mkoa wa Arusha tupo tayari kutoa ushirikiano zaidi kwa taasisi nyingine, pia Wanachama wa Sheria wanafanya kazi kubwa.

Profesa Edward Hosea anazungumza
Rais wa TLS, Profesa Edward Hoseah ambaye pia ni Wakili Mwandamizi na Mwanachama wa TLS anatoa hotuba yake katika mkutano huo.

Profesa Hosea anasema: Chama chetu kilianzishwa Mwaka 1954, kikiwa na majukumu ya kusimamia mienendo na maadili ya wanachama katika taaluma ya Sheria Tanzania.

Profesa Hosea anasema: Chama chetu kilianzishwa Mwaka 1954, kikiwa na majukumu ya kusimamia mienendo ya utendaji na maadili ya wanachama katika taaluma ya Sheria Tanzania, kusimamia utoaji wa elimu endelevu ya Sheria kwa Wanachama wake na kushauri.

Pia kusaidia Serikali, Mahakama na Bunge katika mambo yote ya Sheria na Utawala wa Sheria pamoja na kuwakilisha na kusaidia wanachama katika mambo ya Sheria.

Wiki yote hii tumekuwa na mijadala na mafunzo kwa Mawakili ambapo mada mbalimbali zimewasilishwa ili kuwanoa kulingana na mabadiliko ya teknolojia kwa kuzingatia maadili mema ya taaluma husika.

Kauli Mbiu ya Mkutano wa Mwaka huu ni ‘Kufikisha haki Tanzania, nafasi za taasisi au sekta za Sheria katika utoaji wa haki kwa Taifa’.

Msimamo wa ushirikiano wenye kujenga umetuletea mafanikio makubwa, tumefanikiwa kujenga ushirikiano mzuri na Serikal, Bunge na taasisi nyingine.

Sehemu ya mafanikio hayo ni TLS kupatiwa kiwanja Dodoma na Serikali ya Awamu ya Sita, kiwanja tulichopatiwa ni namba 152 chenye ukubwa wa mita za mraba 9236 katika Mji wa Serikali, Mtumba Dodoma.

Tunaahidi kukiendeleza kiwanja hicho na kukifanya kuwa kutega uchumi na kuhudua kwa wananchi wenye uhitaji.

TLS yaomba kiwanja Arusha
Naomba nichomeke kuwa tunaomba Serikali itupatie kiwanja kwa hapa Arusha ili tuweze kuwekeza.

Rais Samia alitupa nafasi ya kupitia Sheria mbalimbali, TLS tulifanya hivyo kupitia mradi wa AC2 na baada ya hapo iliandaliwa ripoti yenye uchambuzi yakinifu, tunaamini ripoti hiyo itasaidia kuondoa Sheria kandamizi Nchini.

Ushirikiano mzuri kati yetu na Serikali, imewezesha Rais wa TLS kuchaguliwa na kuwemo kwenye kikosi kazi cha Rais kuchambua hali ya siasa nchini na Katiba ya Nchi, hilo ni jambo jema kwa kuwa tumepata nafasi ya kutoa maoni na kuyawasilisha kwa Mheshimiwa Rais.

Kila mwaka mawakili wana uhisha leseni zao au mawakili wapya wanalipa ada ili kupatiwa leseni, kisheria fedha hizo zilitakiwa kurudishwa baada ya Mahakama kukamilisha sherehe za kuwaapisha mawakili wapya.

Kwa muda mrefu fedha hizo zilikuwa hazirudishwi, baadhi zilikuwa zinapelekwa hazina na kutumika katika matumizimengine kinyume cha sheria.

Kutokana na uhusiano mzuri fedha hizo zimekuwa zikirejeshwa TLS kwa mujibu wa Sheria, hadi sasa akaunti zimefunguliwa CRDB na BOT kwa jina la Wakili Collection.

Hali ya Mawakili kukamatwa hovyo imepungua
Miaka michache iliyopita Jeshi la Polisi na baadhi ya vyombo vingine vya dola kuwakamata Mawakili hovyo pasipo kufuata Sheria na wengine kuwanyima hata haki ya kuwasiliana na ndugu zao au Mawakili.

Kwa ushirikiano na Serikali wimb hilo limeanza kutulia, natoa wito kwa vyombo vya dola kuendelea kuwaheshimu Mawakili kwa kuwa ni maafisa wa Mahakamana wana mchango mkubwa.

Maoni ya kisheria Bungeni
Kutokana na mchango wetu tumefanikiwa kuchangia maoni katika vikao mbalimbali vya Bunge vya Katiba na Sheria.

TLS ina kitengo maalum cha kutoa msaada wa kisheria kwa Wananchi wasio na uwezo wa kumudu gharama, kwa Mwaka 2022 jumla ya Wananchi 7,307 wamepatiwa msaada huo wa kisheria, kati yao 321 wamewakilishwa Mahakamani na Wanachama wa TLS bure, 218 wamepatiwa hati ya msaada wa kisheria na kupangiwa Mawakili wa kuwasaidia bure, wengine waliosalia wamepewa muongozo wa kisheria bure, hali hiyo imesaidia kupungua mrundikano Mahakamani.

Pamoja na hivyo, zipo gharama za uendeshaji hasa maeneo ya Vijijini, mfano katika Sheria ha ardhi, miradhi na mikataba, hivyo ili kutimiza kwa nyakati hayo tunaomba Serikali itenge bajeti maalum ya msaada wa Kisheria ili Wananchi wengi wafikiwe.

Hilo likifanyika itapunguza idadi ya watu wanaoenda kuomba msaada wa kisheria katika ofisi za Wakuu wa Wilaya na Wakuu wa Mikoa.

Sisi Wanasheria tunaweza saidia Wananchi wenye uhitaji, tunaomba Serikali itafakari hilo kupitia Wizaraya Katiba na Sheria na Wizara ya Tawala za Mikoa.

Tunaomba kuboresha huduma katika Mahakama za Mwanzo, tunaamini kwa kuweka mfumo Madhubuti na endelevu wa kisheria wananchi wengi watafaidia kwa kuwakilishwa katika Mahakama za Mwanzo ambapo ndipo kuna wananchi wengi wanaofikisha masuala yao ya kisheria.

TLS imeanzisha Kituo cha Kimataifa cha Usuluhishi wa Migogoro (TIAC) ili kusaidia migogoro nje ya Mahakama kitaifa na kimataifa, hivyo ni rai yetu kuwe na maboresho ya matumizi ya usuluhishi ili kupunguza misongamo Mahakamani.

Kuendelea kusimamia na kuheshimu uhuru wa Mahakama, ingawa suala la uhuru wa Mahakama ni la katiba tunatoa rai kwa Serikali hususani viongozi wa kisiasa kuendelea kuheshimu na kuepuka vitendo ambavyo vinaweza kuminya uhuru wa Mahakama.

TLS tunasisitiza uhuru wa Mahakama kwani haitakuwa na tija kama Mahakama hazitakuwa huru kutimiza wajibu wake au maamuzi yake kutotekelezwa.

Matumizi ya Mihuri ya Elekroniki
Ni muhimu kuhimiza matumizi ya mihuri ya kielektroniki katika taasisi zote za Serikali na Binafsi, kwani kwa muda mrefu tumepambana na vishoka ambapo kumekuwa na madhara mengi ikiwemo wananchi kukosa haki na wananchi kupotea fedha zao.

Hali hiyo imesabababisha hata Mawakili waadilifu kukosa kazi na wakati mwingine kuhusishwa na jinai kwa makosa ambayo hawayajatenda.

TLS ilizindua matumizi ya Mihuri ya Kielektroniki Mwaka 2022, mtu ambaye si Wakili hawezi kutumia mihuri hiyo, tunatoa wito kwa taasisi nyingine kutumia mihuri hiyo.


Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango anazungumza
Anasema: Haki ni msingi wa amani na amani ni nguzo muhimu ya mafanikio na maendeleo, nchi isiyo na msingi mzuri wa haki haiwezi kuwa na maendeleo.

Nimefurahishwa na dhima ya mkutano huu ambayo inatukumbusha TLS na taasisi nyingine za Kisheria tunao wajibu mkubwa wa utoaji na upatikanaji wa haki.

Serikali inawapongeza kwa kutoa msaada wa Kisheria kwa wananchi wasio na uwezo, ambapo kwa mwaka mmetoa huduma kwa Wananchi 7,307.

Natoa rai kwa Mawakili na TLS kuendelea kujitoa na kusaidia wananchi wasio na uwezo wa kulipia kesi mahakamani.

Dkt. Mpango: Mawakili mnalalamikiwa mnatoza gharama kubwa
Dkt. Phillip Mpango amesema “Wananchi wanalalamikia gharama kubwa zinazotozwa na Mawakili katika usimamizi wa mashauri.”

Ameongeza “Inasemekana baadhi yenu mnatoa sababu mbalimbali za kuahirisha kesi Mahakamani kwa maslahi yenu binafsi na kuwa sehemu ya tatizo ya kukamilika kwa mashauri, hivyo kusababisha gharama kuongezeka. Natoa rai Mawakili Wasomi muangalie namna ya kupunguza gharama zenu ili haki ipatikane kwa wakati.”

Natoa rai muangalie namna ya kupunguza gharama zenu na kuongeza ushirikiano na Mahakama ili maboresho yaliyofanyika yapunguze muda wa kuendesha kesi Mahakamani na haki inapatikana kwa wakati.

Dkt. Mpango: Kuna Mawakili wanatuhumiwa kuchukua rushwa na kuwageuka wateja wao
Makamu wa Rais, Dkt. Phillip Mpango amesema “Kuna tuhuma baadhi ya Mawakili wanajihusisha na vitendo vya rushwa na udanganyifu kwa maslahi binafsi, inasemekana baadhi yenu mnawasaliti wateja wenu kwa kupokea rushwa kutoka upande wa pili na kuharibu kesi.”

Ameongeza kuwa “Wito wangu wangu kwa Mawakili na Wanasheria wote Nchini ni kuheshimu maadili ya taaluma ya sheria, nawasisitiza TLS na Kamati ya Mawakili kuchukua hatua kali za kinidhamu.”

Atoa maelekezo TLS wapatiwe kiwanja
Natoa maelekezo kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha, John Mongella kuwapatia TLS kiwanja kwa ajili ya uwekezaji.
 
Back
Top Bottom