Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Wiki hii makamu wa Rais na waziri wa mambo ya ndani wakiwa katika shughuli tofauti za kidini wakiwa jukwaani walizungumza mambo ambayo kwa hakika ni kuingilia uhuru wa imani za watu wengine.
Makamu wa Rais aliwanyooshea vidole viongozi wanaojilimbikizia mali pamoja na kuwaaminisha wafuasi wao kwamba wanaweza kupata maendeleo kwa miujiza, Masauni yeye katika shughuli ya makambi ya kanisa la Wasabato alikuwa anaelekeza viongozi wa dini kuhakikisha wanafuata na kuzingatia mafundisho ya kitabu cha dini ili wasije kuingia katika matatizo na serikali na akafikia hadi hatua ya kutolea mfano yaliyomkuta nabii kiboko ya wachawi.
Viongozi hawa hawako sahihi kunyooshea vidole au kutoa maangalizo dhidi ya imani au dini yote hasa inapokuwa tofauti na yao, huku ni kuingilia uhuru wa kidini au imani za wengine.
Makamu wa Rais au waziri wa mambo ya ndani hawajui imani ipi hasa ni sahihi na ya kweli isiyo na upotofu. Wao kama viongozi wanapaswa kuwa neutral ili mradi katiba na serikali vimeruhusu dini na imani zozote kufanya mambo yao kwa uhuru bila kuvunja sheria.
- Waziri Masauni asema anachofanya “Kiboko ya Wachawi” anathibitisha kuwa alikuwa anafanya utapeli