Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Makamu wa Rais wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema baada ya kutumika vya kutosha katika nafasi mbalimbali serikalini, ameamua kukaa kando kwa hiari na kuwaachia wengine waendeleze gurudumu la kumsaidia Rais Samia Suluhu Hassan.
Mbali na umakamu wa Rais, amesema amefanya kazi Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tume ya Mipango, Waziri wa Fedha na Mipango, Benki ya Dunia (WB) na Julai 2025 atafikisha miaka 68, hivyo inatosha.
"Ni uamuzi ambao nimefanya kwa dhati, Watanzania tunakimbilia milioni 64, nina amini kabisa kuna Watanzania ambao ni vijana wanaweza kubeba mzigo wa kumsaidia Rais kikamilifu bila wasiwasi na chaguo lililofanywa na chama chetu ni chaguo sahihi," amesema.
Kupata taarifa na matukio yanayojiri kuelekea uchaguzi mkuu kwa kila mkoa ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Dkt. Mpango amesema hayo leo Jumanne, Februari 2025 jijini Arusha alipofungua kikao kazi cha tano cha Mamlaka ya Serikali Mtandao.
Dkt. Mpango ameomba kupumzika kuendelea na wadhifa huo baada ya awamu hii ya sita kumaliza na Chama cha Mapinduzi (CCM), kimempitisha Dk Emmanuel Nchimbi kuwa mgombea mwenza katika Uchaguzi Mkuu Oktoba mwaka huu.
Soma, Pia: