Suley2019
JF-Expert Member
- Oct 7, 2019
- 2,203
- 5,610
Makamu wa Raisi Dkt. Philip Mipango
Makamu wa Raisi Dkt. Philip Mipango akimwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan katika kilele cha Maadhimisho ya Jubilei ya Miaka 50 ya Kanisa la New Life Outreach iliyofanyika katika kanisa hilo Sakina mkoani Arusha amegusia suala la Wahubiri wa dini kujilimbikizia mali. Akieleza kuhusu jambo hilo Dkt. Mpango amesema:
“Hivi sasa yameibuka mafundisho ya viongozi wa dini yanayowaaminisha wafuasi wao kutegemea miujiza Zaidi ili kupata maendeleo badala ya kufanya kazi kwa bidii na maarifa. Viongozi hao wanawaelekeza waamini wao kwenda kwenye nyumba zao za ibada ili wakaombewe wapate mali ikiwemo magari, nyumba, pesa wanazo zitamani, lakini pia wanaomba kutatuliwa shida zao tunashuhudia kuongezeka kwa wahubiri wanaojilimbikizia fedha na mali binafsi kutokana na sadaka na mauzo ya vitu mbalimbali vya hao watu wanyonge.
Wengi wa wahanga wa mahubiri ya aina hiyo ni wananchi wanyonge wanaokabiliwa na shida au matatizo mbalimbali ya maisha yakiwemo magonjwa, umasikini migogoro katika ndoa, ugumba kukosa ajira na kadhalika”
PIA SOMA- Kwanini Serikali kupitia Wizara ya Nje, wasishirikiane na Wizara ya Nje ya Congo, kumkamata Tapeli alojiita Nabii kiboko ya wachawi?
- Nimeacha kutoa sadaka baada ya kusikia kauli hii ya mchungaji