Juzi baada ya kushtukia mpango wa viongozi wa CCM Wilaya kumpatia kura Dkt. Mwigulu Nchemba mpango huo ulichezwa kwa namna ingine.
Pamoja na kuweka mazingira yote kuwa kura zitahesabiwa kwa uwazi na taratibu zingine zote kufuatwa bado Dkt. Mwigulu alikuwa kishawashawishi viongozi wote wa CCM Wilaya kumpigia debe kwa wajumbe hao ili kujihakikishia ushindi.
Wagombea wengine walikuwa wakihadaiwa hadaiwa tu lakini wajumbe wapiga kura walikuwa wameshasomeshwa na uongozi na baadhi yao huko siku za nyuma walishawahi kupewa hadi fedha za kununua mahindi na wengine boda boda.
Wagombea ambao walitarajiwa pengine wangempa changamoto kubwa Dkt. Mwigulu akina Zaipuna Yona, Kitila Mkumbo, William Shila, Kitandu Ugula, David Jairo, Wastaafu wa Jeshi Kitundu na Kingu walishaliona hilo na kuamua kuacha kuingia kwenye mpambano.
Eng. Jumbe Katala yeye aliingia tu kwenye mpambano akiwa tayari kishajua hawezi kupenya pamoja na kujenga Shule yake ya Sekondari pale Old Kiomboi.
Pamoja na kuwa CCM wanaweza wasifuatilie hili kwa kutaka Dkt. Mwigulu aendelee lakini ukweli utabaki kuwa Dkt. Mwigulu anapata uongozi kwa ubabe na pia anahonga sana wapiga kura kabla ya hata siku za Uchaguzi kufika. Yeye alianza kuhonga miaka mitatu iliyopita, yaani tangu Uchaguzi wa CCM ufanyike mwaka 2017.