Dkt. Mwigulu azungumza na wawakilishi wa SpaceX na Starlink

Habari za Zanzibar

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2024
Posts
651
Reaction score
433
​

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba amezungumza na wawakilishi wa Kampuni za SpaceX na Starlink kuhusu uwekezaji wa kampuni hizo nchini Tanzania katika sekta ya mawasiliano na teknolojia.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt, London, Uingereza, Oktoba 7, 2026, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Angela Kairuki; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Musa Omar; pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo.

​
 
well done waziri mkuu Dr Mwigulu Nchemba πŸ’ͺ
 
well done waziri mkuu Dr Mwigulu Nchemba πŸ’ͺ
Wewe unaweza ukakuta hata hujasoma wanajadili nini hata Starlink hujui inajihusisha na nini?,ila kutokana na kazi yako ya uchawa ukimuona tu waziri mkuu unapita tu kusifiasifia. Huwa najiuliza watu kama wewe na lukas uongozi ukibadilika upepo ukabadilika akaja Farao mwingine asiyewajua mwaweza kufanya kazi gani zaidi ya uchoko!?
 
Gentleman,
relax bas na ujikite kwenye hoja mahususi mezani, bila kua na mihemko useless na wala kujipiga kifua wakati uko pointless na itapendeza zaidi πŸ’
 
Utapeli tu hakuna kitu huo mtandao utafika nchini mpaka tupate serikali inayojali watu wake
 
Gentleman,
relax bas na ujikite kwenye hoja mahususi mezani, bila kua na mihemko useless na wala kujipiga kifua wakati uko pointless na itapendeza zaidi πŸ’
Maneno pekee unayoyajua ya kiingereza, useless, pointless, gentleman, relax na okay. Nina uhakika huwezi kutunga sentensi ya kiingereza iliyonyooka labda utumie AIπŸ˜‚
 
Wameiona hio wanayodai ni connection yake?
 
unasababisha tatizo ili ujisifie eti umesolve, mbona StarLink ipo Rwanda Kenya Uganda na hatujaona viongozi wakuu wa nchi hizo waki-fly kwenda London kuongea na akina Elon Musk!
 
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba amezungumza na wawakilishi wa Kampuni za SpaceX na Starlink kuhusu uwekezaji wa kampuni hizo nchini Tanzania katika sekta ya mawasiliano na teknolojia.

Kikao hicho kimefanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Hyatt, London, Uingereza, Oktoba 7, 2026, na kuhudhuriwa na Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia, Angela Kairuki; Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Musa Omar; pamoja na Waziri wa Mipango na Uwekezaji, Kitila Mkumbo.

 
hivi huwa mnapata wapi nguvu ya kuwajibu hawa watu,....
kwa levo waliyofika hao, si wa kupona tena,....
 
Gentleman,
relax bas na ujikite kwenye hoja mahususi mezani, bila kua na mihemko useless na wala kujipiga kifua wakati uko pointless na itapendeza zaidi πŸ’
gentleman sijui unakatwa we jamaa mngese sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…