Isanga family
JF-Expert Member
- Feb 25, 2015
- 17,080
- 33,076
Mwigulu nadhani ungeangalia hilo kwa mapana zaidi maana wewe upo kwenye kodi mpya mpya kila siku za kudumaza maendeleo nimeshangaa wengine wapo busy kwenye kuitangaza Tanzania kwenye biashara ya utalii na wewe unakuja na kodi kwenye matangazo sidhani kama pana kampuni za utalii zitapata wateja bila kufanya matangazo mtandaoni mmeweka gharama kubwa kwa wageni kuingia mbugani bado mnataka yale matangazo ya kuwapata wageni mchukue hela.
Mgeni anaenda Serengeti analazimika kulipia transit fee ya 70 usd etc anapita Ngorongoro Park achilia mbali kwa kila gari linaloshuka Ngorongoro Crater si chini ya usd 290 mnachukua hata mgeni awe mmoja hapo gharama za mbuga sijaongea.
Punguzeni gharama hizo mnazofikiria kila kukicha mnafanya wageni waende Nchi zingine zenye gharama nafuu na Simba wanapatikana kirahisi.
Utalii ni biashara ya ushindani Dunia nzima mnapoweka mazingira magumu kwa kuongeza kodi hovyo hovyo mnapunguza idadi ya watalii watakaokuja badala ya kuongeza ufanisi ninyi kila kukicha ndio mnapunguza kasi bila kujua...