BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema hadi mwaka 2022 magari 12,012 yaliyotumika (used) hayakuruhusiwa kuingia nchini kutokana na kutokidhi viwango.
Mwigulu amesema Shirika la Viwango Tanzania (TBS) lilikagua magari 43,982 yaliyotumika ikilinganishwa na magari 35,606 yaliyokaguliwa mwaka 2021, sawa na ongezeko la asilimia 23.5.
Kati ya magari yaliyokaguliwa, magari 31,970 yalikidhi viwango vya ubora na kuruhusiwa kuingia na kutumika nchini na magari 12,012 hayakukidhi viwango.
“Ongezeko la idadi ya magari na bidhaa zilizokaguliwa na Shirika lilitokana na kuondolewa kwa vikwazo mbalimbali vya biashara vilivyowekwa na nchi mbalimbali duniani kudhibiti maambukizi ya Uviko-19,”amesema.
Hayo ameyasema leo Alhamisi Juni 15, 2023 akisoma Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa katika mwaka 2022 iliyowasilishwa Bungeni jijini Dodoma.
BUNGENI