ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema Serikali Imezalisha Ajira 547,600 Kwa mwaka kipindi Cha kuanzia July 1 Hadi February mwaka wa Fedha 2022/2023.
Ajira hizo ni kwenye sekta ya umma na sekta binafsi.
Hongera sana Waziri wa Fedha na Serikali ya awamu ya 6 Kwa kupunguza mass employment iliyozalishwa miaka 5 iliyopita.
====
Serikali imeendelea kuratobu masuala ya uzalishaji wa fursa za ajira nchini na hadi February mwaka huu, fursa za ajira 547,031 zimezalishwa.
Haya yamebainishwa na Waziri wa Fedha na Mipango, Dkt. Mwigulu Nchemba wakati wa kuelezea baadhi ya maeneo yaliyopata mafanikip wakati wa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa mwaka 2022/23.
Alisema fursa hizo za ajira zimetengenezwa hususani kupitia utekelezaji wa miradi ya kielelezo, uwezeshajo wa mazingira mazuri ya uwekezaji na kuimarisha sekta binafsi.
Dkt. Mwigulu alisema, kati ya ajira 547,031 zilizozalishwa hadi Februari mwaka huu katika sekta mbalimbali nchini ajira 321,363 zimezalishwa na sekta ya umma ikiwemo utekelezaji wa miradi ya maendeleo na ajira 225,668 zimezalishwa na sekta binafsi rasmi.
Habari Leo