Dkt. Mwigulu Nchemba: Viwanja vitano vya michezo vitawekwa nyasi bandia

Suley2019

JF-Expert Member
Joined
Oct 7, 2019
Posts
2,203
Reaction score
5,610

Nitumie nafasi hii kuwahakikishia Watanzania kuwa tutaweka nyasi bandia kwenye viwanja 5 kwa kuanzia Mwanza, Arusha, Tanga, Dodoma na Mbeya ili kukuza mchezo hapa nchini.

Msamaha wa kodi kwenye nyasi bandia na vifaa ambata vyake utakwenda mpaka ngazi ya Halmashauri".
 
Nanfua a.ka Liti stadium itakosa kweli?
 
Haya ndio maneno tunayotaka kuyasikia bhaana
 
Yaani viwanja vya CCM vinawekwa nyasi Kwa kodi yetu Wananchi
Alafu ili kuwapumbaza akajazia nyama za usimba na uyanga ili mbaki mnabishana huku mitaani msahau mambo ya msingi kwenye hotuba ya bajeti.
 

Aanze na jiji la pili kwa ukubwa Tanzania, MWANZA. Then wafuate wengine...
 
Wanaweka nyasi bandia halafu wakati huo huo TFF wana ndoto za kuomba kuandaa AFCON ya mwaka 2027, na ambapo viwanja vinavyotakiwa kutumika ni lazima viwe na nyasi za asili kama zile za Uwanja wa Benjamin Mkapa, Kirumba Mwanza, Sheikh Amri Abeid Arusha, Sokoine Mbeya, nk!

Au ndiyo wanatengeneza mazingira ya kupiga 10%? Nyasi bandia zina uzuri gani? Na wakati kila siku wachezaji wanazilalamikia kuumiza miguu yao? Kwa nini wasiboreshe pitch kwa kutumia nyasi asili? Kwa nini wasichimbe visima virefu karibu na uwanja kwa ajili ya kumwagili kama hakuna maji ya bomba! Kwa nini hizo pesa zisitumike kuwekea viti na kuboresha majukwaa! Nyasi bandia usawa huu!! Akili za wapi hizi!

Halafu ni lini hivi viwanja vitarejeshwa kwenye Halmashauri zetu ili visimamiwe ipasavyo? Maana hivi viwanja vilijengwa enzi za utawala wa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kwa ajili ya kuwanufaisha Watanzania! Sasa huyu jambazi CCM anavimiliki kwa mamlaka gani?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…