Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ally Mwinyi amehitimisha ziara yake ya Kikazi nchini Zimbabwe na kuagwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Zimbabwe Mhe. Virginia Mabhiza, Balozi wa Zimbabwe nchini Tanzania Mhe. Hellen Bangawe pamoja na viongozi mbalimbali wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwemo Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Balozi Mahmoud Thabit Kombo na Balozi wa Tanzania nchini Zimbabwe Mhe. IGP Mstaafu Simon Sirro.
Mhe. Dkt. Mwinyi alikuwa nchini humo kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika tarehe 20 Novemba, 2024.
Mhe. Dkt. Mwinyi alikuwa nchini humo kushiriki Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) uliofanyika tarehe 20 Novemba, 2024.