Maandalizi yanaendelea kwa ajili ya mapokezi na utambulisho wa mgombea pekee wa urais wa Zanzibar kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Hussein Ali Mwinyi, yatakayofanyika Februari 15, 2025, visiwani Pemba.
Viongozi wa CCM wamesema maandalizi hayo yanakwenda vizuri huku wakieleza kujivunia mafanikio yaliyopatikana chini ya uongozi wa Dkt. Mwinyi. Aidha, wameahidi kumpa zawadi ya wanachama wengi wapya watakaohama kutoka ACT Wazalendo na kujiunga na CCM.
Mapokezi hayo yanatarajiwa kuwa sehemu ya kuonesha mshikamano wa chama hicho kuelekea uchaguzi mkuu ujao, huku viongozi na wafuasi wa CCM wakisubiri kwa hamasa kubwa ujio wa Dkt. Mwinyi kisiwani Pemba.