Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mgombea urais Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dkt Hussein Mwinyi amesema muungano uliopo kati ya Tanganyika na Zanzibar ndio unaleta amani na utulivu katika Taifa.
Amesema Muungano unaleta umoja wa Kitaifa na hivyo Wazanzibari wanaweza kumiliki ardhi na kuwa na shughuli Tanzania bara, kitu ambacho kimeongeza umoja.
Ameongeza kuwa endapi atachaguliwa kuwa Rais wa Zanzibari katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 28 ataendelea kuuenzi Muungano uliopo.
Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuunda Tanzania ambayo inaongozwa na Serikali 2 ambazo ni Serikali ya Mapinduzi Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Ameyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni unaofanyika Mnazi Mmoja, Zanzibar.