Dkt. Nchimbi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mzee Lowassa Kamanda wa Vijana ndio Waliruhusu Vijana Social Kinondoni iwe Bure Kwa Vijana Wote!

Dkt. Nchimbi akiwa Mwenyekiti wa UVCCM na Mzee Lowassa Kamanda wa Vijana ndio Waliruhusu Vijana Social Kinondoni iwe Bure Kwa Vijana Wote!

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Wengi Hawajui Mchango wa Nchimbi Kwa Vijana wa sekta mbali mbali nchini lakini ni huyu Nchimbi ndiye aliruhusu Vijana kutumia ukumbi wa Kinondoni kukuza vipaji vyao bila kujali itikadi za kisiasa

Nakumbuka tukiwa pale Kambi ya Home Alone jirani na Kwa Salva Rweyemamu Mwenyekiti Nchimbi alisema siyo Sahihi Vijana wetu kwenda kucheza show Kwenye kumbi za Disco huko Billicanas na Magot bali tuwatengenezee Mifumo ya Wao kukuza vipaji na kuuza Kazi zao

Siku chache baadae ikatolewa ruhusa ukumbi wa Vijana Social Kinondoni na Ule wa CCM Makangira pale Msasani Namanga Kwa Wassira pawe huru Vijana wetu kuonyesha na kukuza vipaji vyao

Ndio wakaibuka akina Vengu, Masanja, Mrisho Moto, Mwakifwamba, Waukae, anti Ezekiel, Thabit na wengine kibao katika Fani za Sanaa ya maigizo na uimbaji

Kadhalika vikundi lukuki Vya uzalishaji Mali pale Kinondoni vilianzishwa chini ya maelekezo ya Nchimbi

Binafsi namuona Dr Nchimbi akitupaisha Kiuchumi

Ahsanteni Sana 😃😃

Chadema sasa chagueni Mwenyekiti yoyote atatulizwa na Kutulia🐼
 
Mkuu umenikumbusha kitambo Sana Enzi za home alone na eneo lote la vijana social hall, nimeona Hilo eneo lote limevunjwa sijui wanataka kujenga nini
 
Back
Top Bottom