Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Chagueni CCM kwani ndicho chenye ilani bora inayotekelezeka

Pre GE2025 Dkt. Nchimbi: Chagueni CCM kwani ndicho chenye ilani bora inayotekelezeka

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

iamwangdamin

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2015
Posts
864
Reaction score
1,798
CHAGUENI CHAMA CHA MAPINDUZI KWANI NDICHO CHENYE ILANI BORA INAYOTEKELEZEKA - BALOZI NCHIMBI.

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dk Emmanuel John Nchimbi akizungumza kwenye mkutano wa hadhara Katika Viwanja vya Sabasaba Mtwara Mjini amesema Chama cha Mapinduzi ndo kinatekeleza Ilani na kimefanya Vizuri hivyo Wananchi waendelee kukichagua Uchaguzi utakapo fika kuanzia Serikali za Mitaa mpaka Uchaguzi Mkuu.

"Wananchi muendelee kukiamini Chama cha Mapinduzi Ili kielendelee kushika Dola kwani bado tunafanya vizuri Mtwara tu Ilani imetekelezwa kwa asilimia 80 ". Na kusisitiza Wananchi kuendelea kutunza Amani yetu na asitokee Mtu akashawishi kuharibu amani iliyopo Nchini.

Katika ziara hiyo Katibu Mkuu wa CCM ameambatana na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa (NEC), Oganaizesheni, Ndugu Issa Usi Haji Gavu, Katibu wa NEC, Itikadi, Uenezi na Mafunzo, Ndugu Amos Gabriel Makalla na Ndugu Rabia Hamid Abdalla, Katibu wa NEC, Siasa na Uhusiano wa Kimataifa (SUKI).

iamwangdamin
CCM OYEEEEE , CCM MBELE KWA MBELE
20240729_075326.jpg
 
Ndiyo itachaguliwa lakini Ufisadi, Rushwa, Ajira hewa, Mauaji na Utekaji, huduma duni za jamii vinatupa mashaka makubwa.
 
Huku Mtwara hasa Masasi umeme ni wa shida mno. Kila siku lazima umeme ukatwe kwa saa kadhaa. Tatizo hili lina zaidi ya miaka kumi sasa na hakuna suluhu licha ya kuwa gesi inazalishwa huku. Viongozi hamuoni tatizo hili? Hiyo ccm imesaidia nini? Mechi ya yanga na Chiefs jana dakika ya 70 wamekata umeme!!

2. Barabara ya kutoka dar kuja kusini ni mbaya sana licha ya kwamba barabara hiyo ina umri wa miaka 10 hadi 20 kwa baadhi ya vipande. Barabara haifai, ni ya kufumua na kujenga upya
 
Siasa za hivi zinachosha sana. Tunahitaji disruptors siyo watu wa maneno yale yale, miaka nenda miaka rudi.
 
Back
Top Bottom