The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 896
- 1,427
Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi ameonya vikali Wanachama wanaotafuta uteuzi wa udiwani na uwakilishi ambapo Balozi Nchimbi alisema baadhi ya Wanachama wanaotaka nafasi za uongozi wanaanza kupitisha fomu ili watangazwe kuwa Wagombea pekee ambapo amesema wanaofanya hivyo watakatwa majina.
Pia soma: Pre GE2025 - Kupita bila kupingwa kunapenyezwa taratibu na CCM, tutashtuka ya 2020 yakijirudia tena
Akiongea Jijini Dodoma leo February 19,2025 wakati wa ufunguzi wa mafunzo kwa Makatibu wa matawi na kata kutoka Wilaya ya Dodoma Balozi Nchimbi amesema
"Tumeanza kuona matukio ya baadhi ya Wabunge na Madiwani wakipitisha fomu ili watangazwe kuwa Wagombea pekee wengine wanahamasisha vikao kutoa matamko kwamba wapitishwe bila kupingwa, wapo wanaoandaa kumbukumbu za misiba, siku za kuzaliwa na hata sherehe za ndoa, lakini Wahudhuriaji wanapewa posho na wamevaa sare za CCM ili ionekane kama mkutano wa kisiasa"
Pia Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Amesema CCM ina utaratibu wa kufuatilia mwenendo wa Wanachama wake na wale wote wanaoendesha kampeni za chinichini wataenguliwa mapema.
"Wengine wameanzisha NGOs kwa malengo ya kisiasa, wengine wanatumia mbinu za kuwachafua waliopo madarakani kwa sasa, wote hawa tunasema waache mara moja wanapoteza muda na kutufanya tufikirie kuwaengua hatutavumilia mambo haya."