Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Naomba nikiri kwamba Mh. Mbunge ni Mdogo wangu na ni Rafiki yangu pia, amekuwa Mwenyekiti wangu wa UVCCM wa Wilaya ya Meatu wakati nikiwa Mwenyekiti UVCCM Taifa lakini pia wakati nasoma degree ya pili Mzumbe yeye alikuwa anasoma degree yake ya kwanza na hajawahi kuacha kuwa mtatamtata hivi hata wakati tunasoma alikuwa hivihivi mtatamtata ni Mtu ambaye habadiliki”
“Tofauti yake na WanaCCM au Wabunge wengine ni tofauti ipo kwenye Familia yoyote, kuna wakati kwenye Familia mmefikia muda wa kula labda huwa mnakula saa saba mchana, kuna Watoto ikifika saa saba na dakika 5 wanakimbilia mbio chumbani kwa Baba wanauliza chakula bado hata mara 10 hadi Baba anatoka anamzaba kibao anamwambia Mimi sio Mama yako Mimi ndio napika?”
“Kuna wengine wanasikitika au wanakwenda kwa Mama kusema wana njaa na wanaambiwa subiri kidogo kinaiva, sasa Mpina ni aina ya yule Mtoto ambaye asubiri yeye kila saa mbio kwa Baba utafikiri Baba ndiye anapika, sasa Mpina punguza hizo pitia kwa Mama eeh!? pitia kwa Mama sema njaa halafu chakula kinapikwa mnakula”
Soma Pia: Luhaga Mpina amshtaki Spika Tulia na Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa kuondolewa Bungeni kinyume na Sheria
“Kwahiyo sisi Wabunge wote ni Watoto wetu, wale wanaosumbua kupiga hodi kila saa, na wale wanaoanza kulia hata kabla njaa haijaanza, sasa Mpina wakati mwingine sio kwa Baba yake pekee yake hata Mgeni amekuja anawahi kwa Mgeni na kusema mpaka sasa hivi hawajapika” Katibu Mkuu wa CCM, Emmanuel Nchimbi leo October 07,2024 kwenye Jimbo la Kisesa ambalo