Dkt. Ndugulile atoa maelekezo juu ya kuboresha mifumo ya TEHAMA nchini

Dkt. Ndugulile atoa maelekezo juu ya kuboresha mifumo ya TEHAMA nchini

JUMA JUMA

JF-Expert Member
Joined
Jan 5, 2013
Posts
790
Reaction score
964
DKT. NDUGULILE ATOA MAELEKEZO JUU YA KUBORESHA MIFUMO YA TEHAMA NCHINI

Na Faraja Mpina, WMTH, Dodoma

Screenshot 2021-03-31 at 06.52.24.png

Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt. Faustine Ndugulile ametoa maelekezo kwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. Zainab Chaula kuitisha kikao cha wadau wataalamu wa Mifumo ya TEHAMA siku ya tarehe 31/03/2021 kitakachoongozwa na wataalamu kutoka katika Wizara hiyo kwa lengo la kufanya tathmini ya mifumo ya TEHAMA ya kifedha iliyopo nchini.

Akizungumza katika kikao chake na waandishi wa habari katika viwanja vya Bunge jijini Dodoma Dkt. Ndugulile amesema kuwa amechukua hatua hiyo kutokana na Hotuba ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na ripoti ya CAG iliyowasilishwa kwake kuonesha kuna changamoto katika mifumo hiyo na Wizara yake imechukua jambo hilo kwa uzito mkubwa.

“Nimemuelekeza Katibu Mkuu wangu kuchukua hatua za haraka kwa kuitisha kikao cha wadau wataalamu ili kufanya tathmini ya mifumo hiyo, idadi yake, changamoto za utengenezaji, uendeshaji na uendelezaji wa mifumo hiyo hapa nchini pamoja na changamoto ya mifumo hiyo kutosomana na kutobadilishana taarifa”, alieleza Dkt. Ndugulile.

Aidha, alisisitiza kikao hicho kuwahusisha wataalamu kutoka Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi na Utawala Bora, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) ,Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Kituo cha Kuhifadhia Data cha Taifa (NIDC), Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Serikali Mtandao (eGA).

“Natoa wiki moja kwa wataalamu hawa kufanyia kazi jambo kubwa lililogusiwa na Mhe. Rais Samia la uwezekano wa mifumo hiyo kuruhusu mianya ya upotevu wa mapato na usalama wa mifumo hii na kutoa mapendekezo ya maboresho ya nini kifanyike ili kuhakikisha mianya hiyo inazibwa, usalama wa mitandao unakuwepo na kunakuwa na mifumo inayosomana ambayo haitaruhusu kupoteza mapato ya nchi”, alizungumza Dkt. Ndugulile.

Aliongeza kuwa Wizara yake itafanyia kazi mapendekezo hayo ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kuboresha na yale ambayo yatahitaji yatahitajika kushughulikiwa na mamlaka ya juu yatachukuliwa na kupelekwa haya kwa hatua nyingine zaidi.

“Jukumu kubwa la wizara hii ni kutoa miongozo, usimamizi wa mifumo , uendelezaji na kuhakikisha nchi inakuwa na matumizi sahihi ya mifumo ya TEHAMA na salama wake, mifumo mingi iliyokuwa inatumiwa na Serikali ilikuwa inatoka nje ya nchi na fedha nyingi zilitumika kwa uendeshaji na kulipia leseni lakini kwa sasa zaidi ya asilimia 80 ya mifumo inayotumika nchini na ndani ya serikali imetengenezwa na wataalamu wetu wazalendo”, alisisitiza Dkt. Ndugulile.

Alisema kuwa jukumu kubwa alilonalo katika wizara hiyo ni kuhakikisha inajenga uwezo wa wataalamu wa ndani ya nchi kuhakikisha mifumo mingi inaweza kutengenezwa hapa hapa nchini katika ubora unaouhitaji kwa mahitaji ya nchi na usalama dhidi ya udukuzi ambao unaweza kufanyika kwa kutumia mifumo ya iliyotengenezwa mahali pengine.

“Naomba niwaambieni kuwa TEHAMA ni sehemu ya siasa, biashara, ni masuala ya kiusalama na sisi kama Wizara tuna jukumu la kuhakikisha sekta za kiuchumi na fedha zinakuwa na mifumo imara, sekta za huduma ya kijamii kama vile afya, elimu na maji zinakuwa na mifumo salama na sekta zinazohusika na mambo ya ulinzi na usalama nazo zinakuwa na mifumo salama ili hata pale panapokuwa na changamoto kuhakikisha huduma za nchi zinaendelea pasipo kuathirika”, alimalizia Dkt. Ndugulile.

Imetolewa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari
 
Kuboresha mifumo siyo suala la wiki moja ni lazima watu wakae hata zaidi ya miezi 6 ndiyo waje na solution ya kudumu tena wakihusisha na wataalam wa nje kama consultant
 
Mifumo ya TEHAMA ya serikali pasua kichwa inasumbua haijawahi tokeaa hakuna mfumo ambao upo smooth mifumo yote inasumbua
 
Kwani suala la mifumo ya serikali si ni jukumu la eGA ambao wapo ofisi ya raisi utumishi?. Na hawa kama sikosei ndio wenye mamlaka yote juu ya mifumo ya serikali sasa mbona kama wizara ya mawasiliano inaingilia majukumu ya hiyo mamlaka(eGA).

Na hawa ndio wanamiongozo yote. Maana mashirika ya umma yaliyo chini ya wizara ya mawasiliano ni kama TTCL,COSTECH,TCRA TPB n.k.
 
Na pia kama hakuna kubadilishana taarifa kwenye mifumo upigaji lazima uwe mwingi sana na hata kufanya auditing lazima iwe ngumu so ufisadi lazima uwe mwingi pia
 
Mwanaccm umefura kama kifutu na inaonekana humpendi waziri wa mawasiliano na technolojia ya habari. Acha roho mbaya
Nisimpende nami ndie niliyempa kura ccm demokrasia imetamalaq kukosolewa kawaida!
 
Kwahiyo mifumo ya upigaji noti zilizokuwa zinaenda moja kwa moja kwa marehemu Jiwe ndio wanaenda kuipiga chini , too late hivi Mama Samia umetuma watu wakasachi nyumbani kwa Jiwe Kuna vyumba underground vimejaa noti alikuwa anaficha huko .
 
Kuboresha mifumo siyo suala la wiki moja ni lazima watu wakae hata zaidi ya miezi 6 ndiyo waje na solution ya kudumu tena wakihusisha na wataalam wa nje kama consultant

Umeambiwa ni issue ya wiki moja? Tatizo mnasoma tu na sio kuelewa ulichosoma.
Kwa kifupi ni kikao cha kufanya tathmini na mapendekezo.
 
Back
Top Bottom