Dkt. Ndugulile kusuka au kunyoa uchaguzi WHO leo

jjackline

Senior Member
Joined
Jul 25, 2024
Posts
111
Reaction score
274
Mkutano wa Afya wa 74 wa Shirika la Afya Duniani (WHO) unaoendelea Brazzaville, Congo leo Jumanne, Agosti 27, 2024 unatarajiwa kumpitisha Mkuu wa WHO Kanda ya Afrika ambapo miongoni mwa wagombea watano Tanzania inawakilishwa na Dk Faustine Ndugulile.

Wagombea wengine ni pamoja na Dk Boureima Hama Sambo (Niger) Dk N'da Konan Michel Yao (Cote d'Ivoire), Dk Ibrahima Soc'e Fall (Senegal) na Dk Richard Mihigo (Rwanda).

Dk Ndugulile ambaye ni Mwanateknolojia, mtunga Sera, Mwanasiasa na mwakilishi wa wananchi kutoka Jimbo la Kigamboni, Dar es Salaam kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) anawakilisha nchi baada ya kuteuliwa na Rais Samia Suluhu Hassan kuwania kinyang’anyiro hicho.

Soma Pia: Viongozi wa Tanzania Washiriki 'Walk the Talk' Jijini Brazzaville

 
Kumbe sio daktari wa tiba Bali ni mwanateknolojia?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…