Dkt. Ndugulile umetuachia Vodacom kuwa kibanda umiza? Haya sasa makabwela acha tusage lami

Dkt. Ndugulile umetuachia Vodacom kuwa kibanda umiza? Haya sasa makabwela acha tusage lami

mgt software

JF-Expert Member
Joined
Nov 1, 2010
Posts
13,778
Reaction score
7,145
Wana JF,

Vodacom Kwa Sasa rasmi Kibanda umiza. Ukiacha hela kidogo Tu wanaanza kukwambia Asante Kwa kujiunga Sasa endelea kuchagua ili ushinde. Unaweza weka fedha kufungua kifurushi wataficha menu hhuku wakikuwekea fedha Za kiwango cha chini. Upati menu ulizoziona kabla ya kuweka fedha.

Mfano nimeweka 7500 wakata 1200 ambazo nadaiwa. Nikaweka kifurushi cha 5000 badala ya kubaki Na 1300 nimekuta 500 Tu. Hii wamenifanyia mara nyingi, Dr. Nxungulile alihaidi kuzuia uporaji Huu lakini bado. Kwa sasa matumizi ya mpesa ndio use e, wanaokataza fedha nyingi muno.

Naona hata Dr. Nsungulile kwa sasa naye hatoshi apigwe chini Tu.

Ndugu mteja, Tsh 1200 zimetumika kulipia huduma ya Nipige Tafu. Kwa sasa huna deni. Piga *149*01*99# sasa kukopa tena!.

Mchanganuo wa Tsh. 7500 ya muda wa maongezi ni: Gharama: Tsh. 6355.93 VAT:Tsh. 1144.07 Jumla:Tsh. 7500

Hongera!Kifurushi cha Internet Tsh5000 cha MB 3072 kimewezeshwa hadi 2021-04-01. Furahia Facebook yenye PICHA bure ununuapo kifurushi chochote cha data.

Baada ya hapo salio nakiya 500 tu
 
nawe umezidi kukopa kopa
Sio hivyo . Kukopa ni kawaida. Hata bila kukopa unadaiwa deni hewa. Mfano wiki chache zilizopita nimeletewa ujumbe kuwa wamenipa mkopo wa songesha ilihali sikuomba mkopo . Nilipocheki kwenye account yangu ya mpesa sikuona chochote. Nikiweka pesa wanakata. Sasa siweki hata sent tena nione watakata viuno vyao au vipi. Wamegeuka majambazi. Ukiwasiliana nao hawatatui tatizo hata jibu hupati. Ni majizi haya.
 
Waizi sana, me yenyewe nina mda tangu niiweke voda pembeni kwanza.
 
Kwanza ni Dr ndungulile Babu unaharibu majina ya watu,
Pili ni kweli kwamba Vodacom wanaficha menu ya kujiunga na vifurushi hili nakuunga mkononi kabisa,menu Yao ili uipate ni mpaka usage meno muda mwingine unaweza ukaghairi ukajiunga kifurushi ambacho hukuhitaji kabisa,Vodacom jirekebisheni katika hili
 
Hawa voda siwaelewi kabisa yaani GB 1 nimeingia Twitter dakika 20 mb zaidi ya 600 zimekwenda?nimewapigia simu wananiambia nifanye setting ya data usage wakati Siku zote natumia kifurushi hichohicho
 
Back
Top Bottom