Dkt. Ndumbaro Awakumbusha uadilifu UVCCM, Songea

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Songea Mjini Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amewataka vijana wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM) wa Manispaa ya Songea Mjini wawe waadilifu katika utekelezaji wa majukumu ya Chama na maelekezo ya viongozi ili kukiendeleza Chama hicho .

Mhe. Ndumbaro amesema hayo leo Julai 8, 2024 mkoani Ruvuma wakati wa mkutano wa Baraza la Umoja wa Vijana hao ambapo amewataka kuimarisha umoja huo kwa kuongeza idadi ya wanachama.

“Kuweni waadilifu ili kujitengenezea nafasi nzuri za kuaminiwa na chama na Serikali pia epukeni sana kutumiwa na watu kwa maslahi binafsi mnapaswa kukitumikia chama na jumuiya na si vinginevyo” amesema Mhe. Ndumbaro

Mhe. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kuwakumbusha vijana hao wajibu wao kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinashinda katika mitaa yote 95 ya Manispaa ya Songea Mjini.

 
Wangoni acheni umalaya, mmekigeuza CCM kuwa kituo cha kukojoza wake za watu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…