Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Januari 21 ulifanyika Uchaguzi Mkuu CHADEMA kwenye nafasi ya Mwenyekiti na Makamu Wenyeviti kwa Bara na Zanzibar, ambako Lissu alitangazwa kuwa Mwenyekiti mpya CHADEMA, siku hiyo pia ulifanyika Mkutano wa Baraza Kuu la Chama na Lissu akafanya uteuzi wa viongozi, na kati ya waliochaguliwa na Mwanasheria wa CHADEMA, Mjumbe wa Kamati Kuu Dkt. Nshala Rugemeleza.
Kwa wale waliokuwa wanafuatilia sakata la DP World jina hili la Nshala Rugemeleza sio jina geni kabisa. Umaarufu wake ulikua zaidi Juni mwaka 2023 alipojitokeza hadharani kupinga mkataba wa DP World kati ya serikali ya Tanzania na Dubai, mkataba ambao aliuita ni “batili” “kiuhaini” na “haramu”.
Nshala hakuishia hapo kwani alitangaza hadharani kuwa yupo mbioni kufungua kesi kupinga dhamira ya Serikali ya kusaini mkataba huo, kitendo ambacho kilimpa umaarufu sana hasa kwenye mtandao wa X baada ya watu wengi kuunga mkono uamuzi huo.
Siku chache baadae, Nshala ambaye pia ni Rais Mstaafu wa (TLS) alitangaza kuwa maisha yake yapo hatarini baada ya kuarifiwa kuwa kuna mipango ya kutaka kumuua kwa kulikalia kooni sakata la DP World ambapo wanaharakati walijitokeza kuonya na kukemea huu ya vitisho dhidi ya Nshala. Siku chache baadae Ofisi ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) ilimuamuru Wakili Rugemeleza kufika Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar Es Salaam, juu ya kauli zake alizozitoa Julai 3.
Ofisi hiyo ilisema kuwa inafanya uchunguzi juu ya kauli alizozitoa, kauli ambazo zilisambaa kupitia mitandao ya kijamii.
Kwa yeyote anayemfahamu Tundu Lissu, bila shaka atakubali kwamba mtindo wake wa siasa, ni mtu ambaye hapepesi macho, si rahisi kuyumbishwa sio kwa vitisho wala kwa rushwa, tabia ambayo tumeiona pia kwa Dkt. Nshala alivyosimama kidete katika kupinga na kupambana dhidi ya mkataba wa DP World.
- Je, kutakuwa na mwanga kwenye ripoti za CAG kuanza kufanyiwa kazi kwa kila anayetajwa kuhusika kwenye ubadhirifu kukaliwa kooni na hatimaye kuchukuliwa hatua?
- Je, siasa za CHADEMA zinaenda kubadilika kutoka kutukanana ovyo na kufanya character assassination na kuwa na vijana wenye kujenga hoja na kuwakabili wapinzani wao kimkakati kutokana na kuzungukwa na viongozi wenye mipango na weledi?
- Je, katika kipindi hiki ambacho, CHADEMA inashikilia msimamo wao wa No Reform, No Election Dkt. Nshala atasaidia kuleta mabadiliko yatakayopelekea kuwa na uchaguzi huru na haki?

Baada ya kupata intro hiyo (hasa kwa Gen Z wenzangu ambao jina hili lilikuwa geni) uteuzi wa Rugemeleza una maana gani kwa CHADEMA?