Dkt. Nshala: Jaji Hamidu Mwanga amenyang'anywa kesi ya CHADEMA

Mwanamwana

Platinum Member
Joined
Aug 1, 2011
Posts
9,604
Reaction score
22,722
Your browser is not able to display this video.

Mwanasheria mkuu wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema kuwa Dkt. Nshala inarudishwa kwa Jaji mwingine ili aamue kama kesi hiyo ililetwa ndani ya muda au nje ya muda, hivyo Jaji Hamidu Mwanga hizi kesi hazimhusu tena.

Ameyasema leo Aprili 15, 2026 wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya mahakama ya rufani kanda ya Dodoma kutengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyozuia CHADEMA kufanya shughuli za siasa nchini.

Pia soma
 
Tutafika tu acha tuoneshane Makali ameidhalikisha sana Mahakama
 
Wajinga wa kiwango hiki hawajahi kuishi hapo kabla kwenye hii dunia
 
TOKA MAKTABA :

25 March 2026​

John Mnyika Afichua Mapya Zuio la Chadema Mahakama ya Rufaa Dodoma​


Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika, amesema mwenendo wa shauri la marejeo ya kesi ya mgawanyo wa mali za chama umeanza kufichua ukweli kuhusu tafsiri halisi ya amri ya zuio iliyotolewa Juni 10, 2025.

Akizungumza baada ya kusikilizwa kwa shauri hilo Machi 24, 2026 katika Mahakama ya Rufaa Tanzania jijini Dodoma, Mnyika alisema hoja iliyotolewa na Wakili Saidi Marijani kwa niaba ya upande wa kina Saidi Issa Mohamed imethibitisha kuwa zuio hilo lilikuwa na mipaka maalum.

Kwa mujibu wa Mnyika, wakili huyo alieleza mahakamani kuwa zuio la kufanya shughuli za kisiasa lilimhusu Katibu Mkuu wa CHADEMA pamoja na Bodi ya Wadhamini pekee.

Aidha, zuio la matumizi ya mali za chama lilielekezwa kwa Katibu Mkuu, Bodi ya Wadhamini, wafanyakazi walio chini yake, mawakala wake na watu wanaotekeleza majukumu kwa maelekezo yake.

Mnyika amesema kuwa wakili huyo alisisitiza kuwa mtu yeyote ambaye hayuko chini ya Katibu Mkuu hakuwa amezuiwa kisheria kutumia mali za chama au kushiriki shughuli za kisiasa.

Hata hivyo, amesema kauli hiyo inakinzana na msimamo uliowahi kutolewa kwa umma na upande huo mwaka 2025, ambapo walidai zuio hilo liliwahusu viongozi wote wa chama pamoja na wanachama kwa ujumla.

Ameongeza kuwa hata waliwahi kumwandikia msajili wa Mahakama Kuu Tanzania wakidai kuwa CHADEMA wameupotosha umma kuhusu tafsiri ya zuio hilo, hatua iliyosababisha msajili kutoa ufafanuzi kuwa zuio hilo lingeweza kuwahusu viongozi wote.

“Leo wameyaruka maneno yao mbele ya Mahakama ya Rufaa,” amesema Mnyika, akisisitiza kuwa hali hiyo inaonesha wazi kuwa msimamo wa CHADEMA walioutoa mwaka 2025 ulikuwa sahihi.

Amesema maendeleo ya leo mahakamani yanawapa nguvu wanachama na viongozi wa chama hicho kuendelea na shughuli za kisiasa, akisisitiza kuwa hakuna zuio la kisheria linalowazuia wanachama au viongozi kushiriki shughuli hizo nje ya wale waliotajwa moja kwa moja kwenye amri hiyo
 

15 April 2026​

Dodoma, Tanzania​

Mahakama ya Rufani Yarejesha Shughuli za Kisiasa za Chadema​



Picha maktaba


Mahakama ya Rufani Kanda ya Dodoma, Aprili 15, 2026 imetengua maamuzi ya Mahakama Kuu yaliyokizuia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kufanya shughuli za Siasa nchini, kufuatia kesi iliyofunguliwa na Said Issa Mohamed (aliyekuwa Makamu Mwenyekiti wa Chadema Zanzibar), Maulidah Anna Komu na Ahmed Rashid Khamis dhidi ya chama hicho.

Mwanasheria Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Rugemeleza Nshala amesema taarifa zaidi kuhusu hatua hiyo itatolewa baadaye Saa 9:00 Alasiri
 

15 April 2026
Dodoma, Tanzania

TANZANIA COURT OF APPEAL LIFTS BAN HANDED BY THE LOWER COURT ON CHADEMA

View: https://m.youtube.com/watch?v=w8PmJ1MVpmcThe Court of Appeal of Tanzania has set aside a High Court of Tanzania order that barred the major opposition party CHADEMA from engaging in political activities

The centre-right party CHADEMA had taken its battle against a sweeping political ban to the highest court in the country, challenging a controversial injunction imposed by the High court of Tanzania controversial Judge Hamidu Mwanga

CHADEMA previously requested Judge Mwanga to recuse himself, citing his background as a former electoral commissioner for both the Zanzibar electoral Commission ZEC and and the National Electoral Commission NEC. The case has in the lower court been marred by allegations of judicial bias.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…