Dkt. Pesha: Tunatarajia kurusha Setelaiti yetu angani 2025, sasa tumefikia hatua ya matengenezo

informer 06

Member
Joined
May 11, 2024
Posts
66
Reaction score
49
Tanzania kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- (DIT) ikishirikiana na wadau mbalimbali wapo katika mchakato wa maandalizi ya kutengeneza na kurusha Setelaiti angani.

IMG_5574.jpeg
Akizungumzia mchakato huo Julai 25, 2024 wakati akihojiwa na Kituo cha habari cha Channel Ten, Mkurugenzi wa Taaluma Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- (DIT), Dr.Petro Ernest Pesha alisema kuwa tayari wameshafanya upembuzi kujua mahitaji yayohitajika ikiwemo kujifunza kwenye mataifa mengine juu ya namna wanavyoweza kufanikisha suala hilo.

Amesema kuwa wataanza kwa kurusha Setelaiti ndogo (Small Setellite) ambayo itakuwa ina uwezo wa kukusanya taarifa mbalimbali ambazo zitakuwa zikichakatwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

"Itakuwa inafanya (Observation), itakuwa ikizunguka na kukusanya taarifa na kuzileta tunazichakata na kama nilivyosema tumeshafanya mchakato wa kudizaini na tumeshafanya mchakato wa kuona ni vifaa gani vinahitajika kwa sababu baada ya kuidizaini tunakuja kwenye kuitengeneza"amesema

Aliongeza kuwa "Tumeshabainisha tunahitaji vifaa gani na tutavipata wapi na tumeshabaini wadau ambao tutashirikiana nao na mazingira ya kuweza kuitengeneza tumeyakamirisha, kwahiyo sasa tunaingia hatua ya pili kuanza kuitengeneza”

Amesema kuwa malengo yao ni kukamilisha mpango huo ifikapo 2025, kwamba ndani ya mwaka huo Setelaiti inatarajiwa kurushwa angani.

"Na lengo letu ambalo tunatarajia ni kwamba ikienda vizuri mwakani tuweze kurusha settlite kama tutachelewa walau 2026 settliti iweze kuwa angani"amesema Dr. Pesha

Aidha Dr. Pesha amesema kuwa lengo kuja na mkakati huo, ni kufuatia kubaini uwepo wa changamoto mbalimbali zikiwemo za kijamii ambazo zinaweza kutatuliwa na teknolojia Setilaiti, hivyo amedai kuwa baada ya kubaini hilo walifanya tathimini kwa kushirikiana na wadau wakaona waje na mpango huo unaoweza kuleta suluhu kwenye baadhi ya mambo nchini.

Amesema kuwa Setelaiti hiyo ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kukusanya taarifa, wanatarajia italeta tija kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo tija za kiusalama, kiuchumi na kijamii.

Ametolea mfano kuwa itawezesha kubainisha maeneo rafiki ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya kilimo, kubaini maeneo yenye rasilimali ikiwemo madini, amesema kuwa hayo yatafakishwa kupitia taarifa zitakazochambuliwa kupitia picha na taarifa zitakazokuwa zinakusanywa na Setilaiti.

Itakumbukwa Novemba 2022 Serikali iliulizwa Bungeni kuhusu hatua zilizofikiwa Tanzania kurusha Setelaiti zake, ambapo Wiziri ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilieleza kuwa tayari ilikuwa imeanza kuandaa utaratibu wa awali utakaowezesha kuunda na kurusha satelaiti yake angani.
IMG_5575.jpeg
Akizungumzia kwa upande wa Afrika, Naibu Waziri ambaye alikuwa akiwasilisha majibu ya Wizara alisema kuwa hadi (Novemba 2022) Afrika ilikuwa na jumla ya Satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani, na kati ya hizio 41 ni tisa tu ambazo zimetengenezwa na zina taswira ya Kiafarika.

Itakumbukwa kati ya mataifa ya Afrika ambayo tayari yamefanikiwa kutimiza suala la aina hiyo ni Kenya ambayo ilirusha Setilaiti yake kwa mara ya kwanza mwaka 2018.

Soma pia: Tanzania yajipanga kujenga setelaiti yake
 
Amesema kuwa Setelaiti hiyo ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kukusanya taarifa, wanatarajia italeta tija kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo tija za kiusalama, kiuchumi na kijamii.
Utekaji utapungua?
 
Tanzania kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- (DIT) ikishirikiana na wadau mbalimbali wapo katika mchakato wa maandalizi ya kutengeneza na kurusha Setelaiti angani.
View attachment 3063109

View attachment 3063111
Akizungumzia kwa upande wa Afrika, Naibu Waziri ambaye alikuwa akiwasilisha majibu ya Wizara alisema kuwa hadi (Novemba 2022) Afrika ilikuwa na jumla ya Satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani, na kati ya hizio 41 ni tisa tu ambazo zimetengenezwa na zina taswira ya Kiafarika.

Itakumbukwa kati ya mataifa ya Afrika ambayo tayari yamefanikiwa kutimiza suala la aina hiyo ni Kenya ambayo ilirusha Setilaiti yake kwa mara ya kwanza mwaka 2018.
Itasaidia nini kwenye 'Uchumi wa bluu'?
 
Ni ujinga nchi imeunganishwa kwa lami karibia 90 percent halafu watu kuja na hoja mfu kama kubaini sehemu zinazofaa kwa kilimo,hao wakuu wa wilaya,mikoa,maDED sijui wenyeviti wa serikali za mitaa wanaolipwa kwa hela a wananchi wao kazi yao ni nini kwanini wasizunguke kwenye vituo vyao vya kazi kuyajua hayo?

Isiwe kwa sababu Kenya au nchi yoyote Africa walirusha satellite zao na sisi tuige tuangalie yetu ya msingi huko kusema unarusha satellite halafu kuna sehemu huduma za afya mbovu au hazipo kabisa,maji shida zipo sehemu barabara ni mtihani hizo gharama zielekezwe huko.
 
Tanzania kupitia Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- (DIT) ikishirikiana na wadau mbalimbali wapo katika mchakato wa maandalizi ya kutengeneza na kurusha Setelaiti angani.
View attachment 3063109
Akizungumzia mchakato huo Julai 25, 2024 wakati akihojiwa na Kituo cha habari cha Channel Ten, Mkurugenzi wa Taaluma Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam- (DIT), Dr.Petro Ernest Pesha alisema kuwa tayari wameshafanya upembuzi kujua mahitaji yayohitajika ikiwemo kujifunza kwenye mataifa mengine juu ya namna wanavyoweza kufanikisha suala hilo.

Amesema kuwa wataanza kwa kurusha Setelaiti ndogo (Small Setellite) ambayo itakuwa ina uwezo wa kukusanya taarifa mbalimbali ambazo zitakuwa zikichakatwa kwa ajili ya matumizi mbalimbali.

"Itakuwa inafanya (Observation), itakuwa ikizunguka na kukusanya taarifa na kuzileta tunazichakata na kama nilivyosema tumeshafanya mchakato wa kudizaini na tumeshafanya mchakato wa kuona ni vifaa gani vinahitajika kwa sababu baada ya kuidizaini tunakuja kwenye kuitengeneza"amesema

Aliongeza kuwa "Tumeshabainisha tunahitaji vifaa gani na tutavipata wapi na tumeshabaini wadau ambao tutashirikiana nao na mazingira ya kuweza kuitengeneza tumeyakamirisha, kwahiyo sasa tunaingia hatua ya pili kuanza kuitengeneza”

Amesema kuwa malengo yao ni kukamilisha mpango huo ifikapo 2025, kwamba ndani ya mwaka huo Setelaiti inatarajiwa kurushwa angani.

"Na lengo letu ambalo tunatarajia ni kwamba ikienda vizuri mwakani tuweze kurusha settlite kama tutachelewa walau 2026 settliti iweze kuwa angani"amesema Dr. Pesha

Aidha Dr. Pesha amesema kuwa lengo kuja na mkakati huo, ni kufuatia kubaini uwepo wa changamoto mbalimbali zikiwemo za kijamii ambazo zinaweza kutatuliwa na teknolojia Setilaiti, hivyo amedai kuwa baada ya kubaini hilo walifanya tathimini kwa kushirikiana na wadau wakaona waje na mpango huo unaoweza kuleta suluhu kwenye baadhi ya mambo nchini.

Amesema kuwa Setelaiti hiyo ambayo itakuwa maalumu kwa ajili ya kukusanya taarifa, wanatarajia italeta tija kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo tija za kiusalama, kiuchumi na kijamii.

Ametolea mfano kuwa itawezesha kubainisha maeneo rafiki ambayo yanaweza kutumika kwa ajili ya kilimo, kubaini maeneo yenye rasilimali ikiwemo madini, amesema kuwa hayo yatafakishwa kupitia taarifa zitakazochambuliwa kupitia picha na taarifa zitakazokuwa zinakusanywa na Setilaiti.

Itakumbukwa Novemba 2022 Serikali iliulizwa Bungeni kuhusu hatua zilizofikiwa Tanzania kurusha Setelaiti zake, ambapo Wiziri ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, ilieleza kuwa tayari ilikuwa imeanza kuandaa utaratibu wa awali utakaowezesha kuunda na kurusha satelaiti yake angani.
View attachment 3063111
Akizungumzia kwa upande wa Afrika, Naibu Waziri ambaye alikuwa akiwasilisha majibu ya Wizara alisema kuwa hadi (Novemba 2022) Afrika ilikuwa na jumla ya Satelaiti 41, na kuanzia mwaka 2016 ni satelaiti 20 tu ambazo zimekuwa angani, na kati ya hizio 41 ni tisa tu ambazo zimetengenezwa na zina taswira ya Kiafarika.

Itakumbukwa kati ya mataifa ya Afrika ambayo tayari yamefanikiwa kutimiza suala la aina hiyo ni Kenya ambayo ilirusha Setilaiti yake kwa mara ya kwanza mwaka 2018.
kwenye hiyo project kama sitashirikishwa hakuna kitu kitaruka hapo 2026 labda hadi 2033
 
Watatumia manati kuirusha? By the way ni kwa elimu hii ya kibongo au kuna nyingine.
 
Back
Top Bottom