Dkt. Philip Mpango: Jitihada zinahitajika kutoa elimu ya magonjwa yasioambukiza

Dkt. Philip Mpango: Jitihada zinahitajika kutoa elimu ya magonjwa yasioambukiza

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
Bohari ya Dawa (MSD) imeshiriki Mkutano wa Kimataifa wa Magonjwa ya Moyo ulioandaliwa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete na kuwakutanisha Madaktari Bingwa, wataalam na wadau wa afya, wauguzi na watunga sera kutoka mataifa zaidi ya 40 Duniani kwa lengo la kujadiliana na kubadilishana uzoefu katika masuala mbalimbali yanayohusu magonjwa ya moyo Duniani, Februari 9, 2024.

Akifungua Mkutano huo wa siku mbili unaofanyika katika Ukumbi wa Golden Tulip Airport – Unguja, Zanzibar.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango amesema jitihada zinahitajika katika kutoa elimu ya magonjwa yasioambukiza pamoja na kuzingatia mtindo bora wa maisha, mazoezi na kufanya vipimo vya afya mara kwa mara ili kukabiliana na maradhi mbalimbali ikiwemo magonjwa ya moyo.
IMG_20240210_134553_921.jpg
Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Mavere Tukai akipokea Tuzo Maalum kutoka Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango, iliyotolewa na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), kwa kutambua mchango wa MSD katika kuhakikisha bidhaa za afya zinazohusisha na huduma, dawa na vipimo vya magonjwa ya moyo, zinapatikana nchini.


Amesema katika kukabiliana na ugonjwa wa moyo ni muhimu wananchi kufuata njia za kujikinga zaidi ikiwemo kuacha ulevi uliyopindukia, uvutaji sigara, tabia bwete pamoja na uzito uliyopindukia. Ametoa rai kwa watalaamu wa afya, wasomi, vyombo vya habari pamoja na watunga sera kushiriki katika utoaji elimu kuhusu masuala ya afya.
IMG-20240210-WA0007.jpg

IMG-20240210-WA0008.jpg

IMG-20240210-WA0010.jpg
Aidha, Makamu wa Rais amesisitiza kuwa tafiti zinapaswa kufanyika kwa kina ili kubaini visababishi zaidi vya magonjwa ya moyo kwa kupata taarifa zaidi juu ya taratibu za kijamii na tabia za kiutamaduni katika mambo mbalimbali yaliyozoeleka kufanyika barani Afrika.

Mbàli na kushiriki mkutano huo, MSD imepokea tuzo maalum kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete, kufutia mchango wake katika kuhakikisha bidhaa za afya zinazohusisha na dawa na vipimo vya magonjwa ya moyo, zinapatikana nchini.
 
Shirikisho la wafanyakazi limesema Mkoa wa Arusha chini ya RC Makonda umevunja rekodi ya kufanikisha Sherehe za Mei Mosi kwa Viwango vya Juu kabisa

Source TBC
 
Kweli kila mtu ana priorities zake. Sasa uzuri wa sherehe ya siku moja utakusaidia nini ewe mfanyakazi siku 364 na robo zilizobakia?
 
Ukiona mtu anamsifia mwanasiasa tiashaka
 
Huyu MWAMBA Chaggadema wamuache tu huyu mtu ni chaguo la Mungu.Mungu ameamua kumwinua juu sasa hivi sisikii tena nafasi ya Katibu mwenezi Taifa.Makonda ni Arusha na Arusha ni Makonda
 
Back
Top Bottom