Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Dkt. Pindi Chana ameshiriki hafla ya usiku wa Mwanamke, Machi 08, 2023 iliyowahusisha Wanawake wa Mkoa wa Njombe ambapo shughuli mbalimbali zikiwemo za ubunifu wa mavazi na elimu ya ujasiriamali zimepamba hafla hiyo.
Hafla hiyo ni katika maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani ambayo Kitaifa imeongozwa na Kauli mbiu Mabadiliko ya Teknolojia ni chachu katika kuleta usawa wa kijinsia.