Adilinanduguze2
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 1,386
- 1,919
DR. SALIM AHMED SALIM NI MTU WA AINA GANI?
Heri ya mwaka mpya wadau wa Uwanja wa Diplomasia.
Poleni kwa kimya kirefu.
Leo tunawaletea maelezo kuhusu mwanadiplomasia nguli wa Tanzania ambaye ni kiigizo (Role model) cha ndugu yetu Abbas Mwalimu,huyu si mwingine bali ni Dr. Salim Ahmed Salim.
Mara baada ya kuundwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania hapo mwaka 1964, Mambo ya Nje ni moja ya mambo yaliyokubalianwa kuwa yawe ya Muungano, hivyo nafasi kama za Ubalozi katika Nchi mbalimbali Washirika na Taasisi za Kimataifa ilibidi zigawanywe kati ya Watanganyika na Wazanzibari ili dhana ya Utanzania ipate kuonekana dhahiri.
Ni katika wakati husika ndipo Rais Julius Nyerere, Kama Mkuu wa Nchi na mtu mwenye Mamlaka ya Uteuzi wa Mabalaozi alipoomba majina ya wale ambao walionekana kuwa na sifa za kuteuliwa kuwa Mabalozi kutoka Zanzibar kwa Rais Abeid Amani Karume.
Miongoni mwa majina yaliyoletwa na Sheikh Karume kwa Mwalimu Nyerere ni jina la Kijana mdogo wa miaka 22 Salim Ahmed Salim, jambo ambalo lilimfanya Mwalimu Nyerere amuulize mara ya pili Rais Karume juu ya umri wa Kijana huyo, majibu aliyopewa ni kuwa huyo ni Kijana wa Zanzibar mwenye vigezo na uwezo, apewe nafasi.
Bila hiyana, Mwalimu Nyerere akamteua Kijana huyo Salim Ahmed Salim kuwa Balozi wa Tanzania katika Jamhuri ya Uarabu ya Misri, nafasi ambayo aliitumikia kwa muda wa Mwaka mmoja kati ya Mwaka 1964 na 1965 kabla ya kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania Nchini India.
Unaweza kudhani kuwa Salim Ahmed Salim alipewa nafasi husika kwa upendeleo, au kwa kuwa Chama chake cha Ummah Party kilikuwa na mahusiano ya karibu na Chama cha ASP cha Karume.
Uwezo wa Dkt Salim Ahmed Salim katika kuieneza Diplomasia ya Tanzania kwa muda wa miaka 50 ya Muungano wetu unaonyesha dhana ya upendeleo isivyo na mashiko, lakini hata uzoefu na Ukindakindaki wake wakati akiteuliwa kushika nafasi hiyo pamoja na kuwa alikuwa na umri mdogo vinaonyesha kuwa aliistahili nafasi hiyo.
Dr. Salim hakuwa mgeni wa Siasa za Zanzibar, alichipukia katika Chama cha Zanzibar Nationalist Party, ZNP chini ya ulezi wa Komredi mahiri, Profesa Abdulrahman Mohammed Babu na bega kwa bega naye alishiriki katika kukiasisi Chama cha Kwanza chenye kufuata Mrengo wa Kijamaa katika Afrika, Chama cha Ummah Party, Chama ambacho kilishirikiana na Chama cha ASP katika kutekeleza Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 yaliyomuingiza madarakani Karume.
Ni Chama hiki cha Ummah Party ndicho kilichotoa wanamapinduzi Majemedari kama Komredi Ali Sultan Issa, Kanali Ali Mahfoudh, Komredi Sharifu Ahmed Badawyi Qullatein na wengineo ambao walikuwa chachu ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kijana mdogo Salim Ahmed Salim alishirikiana na kulelewa na wote hao, jambo lililompa uzoefu, uwezo na mafunzo.
Mpaka leo rekodi zinamuonyesha Dkt Salim A Salim aliyezaliwa Januari 23, 1942 kuwa ndiye Mtanzania mwenye umri mdogo zaidi kuteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nje ya Nchi.
Dr. Salim Ahmed Salim hakuishia kuwa Balozi wa Tanzania nchini Misri tu bali alihudumu katika nchi nyingine kama vile India na China.
Pia alihudumu kama Mwakilishi wa kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa kuanzia mwaka 1970.
Mwaka 1976 alihudumu kama Rais wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa kingereza United Nations Security Council (UNSC) na mwaka 1979 kama Rais wa Kikao cha 34 cha Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa (Thirty-Fourth Session of the United Nations General Assembly) UNGA.
Alirejea Tanzania na kuhudumu kama Waziri Mkuu na Naibu Waziri Mkuu kati ya miaka ya 1984 na 1989.
Dr. Salim Ahmed Salim pia alihudumu kama Katibu Mkuu wa iliyokuwa Jumuiya ya Muungano wa Afrika kwa kingereza Organisation of African Unity (OAU) sasa Umoja wa Afrika (AU) kutoka mwaka 1989 mpaka 2001.
Dr Salim Ahmed Salim alihusika kimamilifu katika mabadiliko ya taasisi hii muhimu kwa Afrika kutoka OAU kwenda AU.
Akiwa Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Umoja wa Mataifa ya kuondoa Ukoloni yaani United Nations Special Committee on Decolonisation (UNSCD) Dr Salim Ahmed Salim alisaidia kuweka misingi mipya ya kupatikana kwa kipindi kingine cha Uhuru wa Bara zima la Afrika.
Akiwa kiongozi wa mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi alihudumu kama Mwenyekiti wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liliweka vikwazo dhidi ya Rhodesia kwa kingereza Chairman of the United Nations Security Council Commission on Sanctions against Rhodesia (Sasa Zimbabwe).
Pia alihudumu kama Rais wa Mkutano Mkuu wa Kimataifa ulioiwekea vikwazo nchi ya Afrika ya Kusini kwa kingereza the President of the International Conference on Sanctions against South Africa na pia kama Rais wa Mkutano wa Kimataifa wa Paris uliojadili ubaguzi wa rangi yaani President of the Paris International Conference on Apartheid.
Kwa kutambua mchango wake katika bara la Afrika, Dr. Salim Ahmed Salim alitunukiwa tuzo mbalimbali kutoka katika nchi za Togo, Rwanda na Liberia.
Kwa sasa Dr. Salim Ahmed Salim ni Mwenyekiti wa Taasisi ya Mo Ibrahim Foundation ambayo hutoa Tuzo kwa viongozi bora barani Afrika.
Uwanja wa Diplomasia.
Maelezo haya ni kwa hisani ya Mzee Mohamed Said na tovuti ya Mo Ibrahim Foundation.
Sent using Jamii Forums mobile app