BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
DKT. SAMIZI AENDELEA NA ZIARA JIMBONI, ACHANGIA UJENZI WA VYOO, CHUMBA CHA KUJIFUNGULIA KINAMAMA N.K.
Mbunge wa Jimbo la Muhambwe mkoani Kigoma Mhe. Florence George Samizi ameendelea na ziara yake ya kutembelea miradi mbalimbali Jimboni na kuchangia fedha ujenzi huku akisikiliza kero za wananchi na kuzijibu.
Akiwa Kata ya Itaba ametembelea Shule ya Msingi Kaharawe ambapo amechangia Milioni 3 ujenzi wa vyoo vya wanafunzi pamoja na kuchangia pia Milioni 3 kwenye ujenzi wa chumba cha kujifungulia Kina Mama katika zahanati ya Minyinya.
Dkt. Samizi ametembelea pia Greenhouse ya kilimo cha Mbogamboga na kujionea shughuli mbalimbali zinazofanyika. Mbunge Samizi anaendelea na ziara yake Jimboni kukutana na wananchi kuwaeleza utekelezaji wa Ilani ya CCM, kusikiliza kero za wananchi na kuzitatua pamoja na kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ya maendeleo.
#MuhambeKaziInaendelea
#TunaImaninaSamia