Bilionea wa Jiji la Dar es Salaam ambaye kwa sasa amekuwa gumzo Dkt Louis Shika aliyejizolea umaarufu baada ya kuibuka mshindi katika mnada wa nyumba za mfanyabiashara maarufu, Said Lugumi, Desemba 9, mwaka huu ameandaliwa usiku wake maalum ambao ataongea na Watanzania juu ya maisha yake.
Wakizungumza na waandishi wa Habari mapema leo Novemba 30,2017, Jijini Dar es Salaam, Meneja wa Dkt. Shika, Catherine Kahabi aliweka wazi kuwa wamekuja na wazo hilo la kuandaa tamasha maalum ili watu wote wamtambue Dkt Shika kama mmoja wa watu wakubwa ambao wameweza kuibuka katika mazingira ya chini na baadae kuwa gumzo kila kona.
“Usiku wa 900 Itapendeza ni usiku maalum ambao unatarajiwa kufanyika Desemba 9, mwaka huu. Watu wote wanakaribishwa pale ndani ya uwanja wa burudani, Dar live. Usiku huo ni maalum na Dkt Shika ataweka wazi kila kitu pamoja na historia yake alianzia wapi mpaka kufika Nchini Urusi na baadae kurejea Tanzania” amesema Catherine Kahabi ambaye ni Meneja wa Dkt Shika
Pia aliongeza kuwa, kwa sasa wanamuangalia Dkt Shika kama ni mmoja wa Watanzania wenye bahati na muonekano wa tofauti licha ya kila mmoja kusema lake.
Pia mbali na Dkt Shika, kutakuwa na burudani mbalimbali zitakazosindikizwa na bendi ya Twanga Pepeta, Jahazi Modern Taarab na wasanii wengine kibao wakiwemo wa Bongo fleva na wachekeshaji akiwemo MC Pilipili.
Kwa upande wake msimamizi wa masuala ya burudani wa Dar Live, Rajabu Mteta (KP Mjomba) amesemalieleza kuwa usiku huo utapamba na shamrashamra mbalimbali kwani utakuwa ni wa aina yake kwa kila mmoja atakayefika siku hiyo.
“Wengi bado wapo njia panda kuhusiana na ukweli wa mabilioni ya Dkt Shika. Tumeshuhudia hivi karibuni amelipia bima fedha zilizopo nje ya nchi. Kabla fedha hizo hazijatua ameona atoe kwanza sapraizi kwa wananchi ambapo ukija Dar Live utaishuhudia,” amesema Mteta KP Mjomba.
Usiku huo pia unatarajiwa kuwa na mgeni rasmi ambaye atafungua hafla hiyo, Mkurugenzi wa Global Group, Erick Shigongo kama mtu aliyechangia kwa namna moja ama nyingine kumfanya Dkt Shika kuonekana mtu katika watu kupitia vyombo vyake vya habari ikiwemo Global Tv.