Mpigania uhuru wa pili
JF-Expert Member
- Apr 12, 2023
- 3,380
- 6,376
Miaka 10 iliyopita dr slaa alikua ni mwanasiasa wa upinzani maarufu hakuna aliyemfikia na dr slaa ni moja ya watu aliowafanya watu wengi hasa vijana kupenda siasa za upinzani
Baada ya miaka 15 kupita dr slaa sio relevant tena ule umaarufu hana tena, maisha yana enda kasi sana leo hii ananyimwa dhamana lakini husikii kelele nyingi kutoka kwa wananchi kwamba atoke ni kama jamii a.k.a hadhira imempoteze hii imesababishwa na mambo yafuatayo;-
Baada ya miaka 15 kupita dr slaa sio relevant tena ule umaarufu hana tena, maisha yana enda kasi sana leo hii ananyimwa dhamana lakini husikii kelele nyingi kutoka kwa wananchi kwamba atoke ni kama jamii a.k.a hadhira imempoteze hii imesababishwa na mambo yafuatayo;-
- Usaliti- mwaka 2015 dr slaa aliamua kujitoa chadema na kumuunga mkono magufuli, kwenye point ya kwanza alikua sahii kwa sababu ya maumivu makali ya kusalitiwa na mbowe ila point ya pili ndo mzizi wa kosa alilofanya mpaka leo linamgharimu kumuunga mkono magufuli kwa lugha alikua anaiunga mkono ccm- tafsiri yake ni kwamba dr slaa aliisaliti mpaka dhamira yake mwenyewe kwa sababu dr slaa alikua maarufu kwa kuiponda ccm na watu wake leo hii unarudi na kukaa upande wa ccm usaliti alioufanya ndo matunda yake anayaona leo
- Tukio la kupigwa risasi lisu- dr slaa aliulizwa juu ya tukio la lisu kupigwa risasi alitoa majibu ya hovyo sana ni bora angekaa kimya yale majibu yaliuzi watu sana alifanya vile akijua sponsor wake magufuli ataendelea kutawala
- Tukio la ugaidi la mbowe- dr alisema anakasirika sana pale anaposikia watu wanalalamika kwamba mbowe sio gaidi anayetoa kauli hii ni mtu aliyekaa na mbowe zaidi ya miaka 15 lakin anaongea ujinga kama huu na utuuzima ule
- Kuacha siasa- baada ya kurudi Tanzania na kumaliza ubalozi dr slaa alisema ataacha siasa ghafla kwenye sakata la dp world na bandari anaibuka kutoka mafichoni yes anahaki hiyo ila alisahau anaenda kinyume na mwajiri wake wa zamani ambaye serikali ya ccm na hata kinachomtokea ni kama mwajiri wake kaamua kumkomoa