Dkt. Slaa: Freeman Mbowe aachane na Maridhiano maana hayafai, Katiba sio mali yake binafsi au mali ya Rais Samia

Huyu mzee akae kimya, yaliyotokea awamu ya 5 yalisababishwa na yeye la sivyo tungekuwa na awamu nzuri yenye kuwafanya watu kiendelea kupendana nadala yake ilikuwa awamu ya kiwagawa Watanzania kwa Imani, Ukanda, Makabila nk.
ndipo shida ya wewe mtanzania mjinga inapoanzia mnatafuta makosa na sio hoja za ntu husika mi na sema hv tatz sio viongozi tulionao tatz sio katiba tatizo ni watu wapuuz kama wewe
 
Kwa hiyo Walimu au Wamachinga ndiyo wawaundie Katiba mpya siyo?
 
Mimi kama mimi sina imani kabisa na Mbowe kwa sasa, ila hata hivyo Slaa anaweza kudai katiba mpya bila kurejea CDM. Ama unataka kusema ili uweze kudai katiba mpya ni lazima uwe ndani ya CDM?
Umemkataa Mbowe tangu uchaguzi uliopita ndani ya chama. Kwa taarifa yako bila Mbowe unayemchukia sana, usingekuwa na Chadema leo. Hakika angekuwa kiongozi mwingine, Chadema ingekufa ndani ya miaka ya awamu iliyopita.
 
Marodhiano ni jambo jema kabisa. Lakini jambo lolote lisilo na utaratibu ulioanishwa wazi na muda wa kulitekeleza, linakuwa halina maana, tena linaweza kutafsiriwa kuwa ni hadaa.

Lazima kuwepo na mwongozo ulio wazi. Mathalani:

1) Maridhiano yanahusisha maeneo gani.

2) Nani washiriki wa hayo maridhiano.

3) Yanatakiwa kukamilika lini.

4) Utekelezaji wa hayo maridhiano unaanza lini na kukamilika lini.

5) Yeyote akikiuka hayo maridhiano kutatokea nini.

6) Kama maridhiano yanahusisha upatikanaji wa katiba mpya, lini wananchi wote watahusishwa, watahusishwa kwa namna gani, lini mchakato wa kupatikana katiba mpya utaanza na utakamilika lini.

Mambo haya ni lazima yawe bayana. Vinginevyo inawezekana kutafsiriwa kuwa ni hadaa kwa umma.
 
Hapana! sikupingi, ni kweli inawezekana Mbowe amekuwa na mchango mkubwa kwa mafanikio binagsi ya Slaa lakini pia Slaa amekuwa sehemu ya Mafanikio ya CHADEMA.

Naomba kukuweka sawa kwamba Slaa aliingia CHADEMA mwaka 1995 kabla Mbowe hajawa Mwenyekiti na Mkapa hajawa Rais. Slaa ni Mbunge wa kwanza kabisa wa CHADEMA wa kuchaguliwa kupitia jimbo la Karatu mwaka 1995 akimtoa mkongwe PATRICK QORRO. Hivyo, Mkapa anakuja kuukwaa Urais wa nchi hii, Slaa tayari yupo CHADEMA.
 
Kwa hiyo Walimu au Wamachinga ndiyo wawaundie Katiba mpya siyo?
Huna uelewa wowote Kaa kimyaa, kwani wasomi wote ni viongozi wa vya ma vya siasa? Hata ikitokea ivooo, unafikiri washiriki wa katiba ni hao walim na machinga wote kwani nao ni sehem ya wananchi, katiba ya wananchi ni zao na takwa la Kila raia na kuheshim mawazo ya Kila raia mwenye akili timamu, sio wanasiasa na vyama vyao. Au katiba isitokane na takwa la kikundi chochote Cha kisiasa, tukumbuke katiba ni ni Sheria mama Kwa raia wote na Kwa vyama vyao
 
Ni sawa. Hta hivyo hana sababu ya msingi ya kumshambulia Mbowe aliyekuwa mkuu wake kwenye chama. Alidai amestaafu siasa. anamaze au atangaze kurudi.

Hata kibinadamu, maisha ya kawaida mtu aliyekusaidia hata akikukosea ni vyema ukanyamaza kimya maana hujui kesho itakuwaje. Inaonekana anamchukia mbowe kama vile waligombania mwanamke
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na mariziano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Mwanzoni walikuwa wanasema Wananchi hawataki katiba mpya ila chadema ndiyo wanataka katiba mpya, sasa wamegeuka wanasema katiba mpya ni ya wananchi na siyo mali ya Chadema, sasa kipi ni kipi [emoji848][emoji848][emoji848]
 
Chadema wakiipata msijesema siyo mali yao
 
Hakuna mtu kamzuia Slaa kutafuta katiba mpya, Kama Mbowe anatafuta na mariziano, yeye atafute ya ugomvi, hakuna kupangiana, kila mtu na department yake.
Kwani hukumuelewa nini Dk Slaa?
Katiba sio mali ya Samia na Mbowe,bali ni mali ya watanzania.

Walior8dhiana ni Mbowe na Samia na sio watanzania na Samia!
 
Wewe unayeelewa ni msomi gani aliyejitokeza kwenye swala la muundo wa nchi,maendeleo ya nchi bila kuwa mwanasiasa?
 
Haya maridhiano ni ushetani tupu
 
Huyu mzee akae kimya, yaliyotokea awamu ya 5 yalisababishwa na yeye la sivyo tungekuwa na awamu nzuri yenye kuwafanya watu kiendelea kupendana nadala yake ilikuwa awamu ya kiwagawa Watanzania kwa Imani, Ukanda, Makabila nk.
Sahivi kuna udini mkali sn teuzi zote ni Tanga, Pwani na Zanzibar
 
Mbowe ametuuza mchana kucha. Mbowe astaafu amuachie hardliner chama. Mambo ya kunikomba ikulu na kupiga picha kwenye futari ni ujinga wa Hali ya juu. Atoke Mbowe atoke Mbowe. Chama kirudi kwenye misingi yake ya confrontational politics.
Anzisha chako ili upunguze makasiriko
 
Umemkataa Mbowe tangu uchaguzi uliopita ndani ya chama. Kwa taarifa yako bila Mbowe unayemchukia sana, usingekuwa na Chadema leo. Hakika angekuwa kiongozi mwingine, Chadema ingekufa ndani ya miaka ya awamu iliyopita.

Kwahiyo Mbowe angekufa na CDM ingekufa? Ukiona uhai wa taasisi unategemea mtu fulani ili iendelee kuwepo, kama ni kweli CDM inamtegemea Mbowe ili iendelee kuwa hai, basi ujue hakuna taasisi hapo.

Na kwa taarifa yako nyie ndio mnaochangia hiyo CDM kuonekana ni chama cha mtu, au kikabila kwa utetezi huu. Hata wapambe wa Nyerere walikuwa wanamdanganya kuwa bila yeye kuwa rais, Tanzania haiwezi kuwepo. Leo hii Nyerere hayuko madarakani wala hai, je Tanzania imepotea? Nakushauri, pigania taasisi na sio mtu. Inshort muda wa Mbowe kuendelea kuwa mwenyekiti wa CDM umepita.
 
Kwani hukumuelewa nini Dk Slaa?
Katiba sio mali ya Samia na Mbowe,bali ni mali ya watanzania.

Walior8dhiana ni Mbowe na Samia na sio watanzania na Samia!

Wewe umekatazwa kuanzisha Chama chako ukafanya unachotaka? Au unahangaisha wenzako wenye malengo tofauti
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…