Mkuu sikujua kwa uelewa wetu humu hili la Dr. Slaa kusema kule Marekani katiba yao ina ruhusu kumshitaki rais mstaafu kwa mjibu wa clip ya Jambo TV. Kwenye hiyo barua inaonyesha hakuna rais mstaafu wa Marekani alishawahi kushitakiwa mahakamani ila wanajaribu kufanya hivyo kwa Bw. Trump.
Aidha kwa utafiti wangu hakuna katiba yoyote duniani inaruhusu kumshitaki rais kwa mambo aliyoyafanya wakati anatekeleza majukumu yake kwa mjibu wa katiba na kiapo chake. Hata hivyo rais mstaafu anaweza kushitakiwa kama amefanya kosa jingine lolote kama ambayo Bw. Trump kashitakiwa kwa kosa la nyanyaso la kinjinsia