Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Kesi ya kusambaza taarifa za uongo katika Mtandao wa X inayomkabili mwanasiasa mkongwe nchini, Dk Willibrod Slaa (76) itatajwa leo Jumatano, Februari 19, 2025 katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Dk Slaa anadaiwa kutenda kosa hilo chini ya kifungu cha 16 cha Sheria ya Makosa ya Mtandao namba 14 ya mwaka 2015.
Kesi hiyo ambayo inasikilizwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Beda Nyaki, imeitwa leo Jumatano, Februari 19, 2025 katika Mahakama hiyo kwa ajili ya kutajwa na kuangaliwa iwapo upelelezi wa shauri hilo umekamilika au la.
Hata hivyo, Hakimu Nyaki kwa sasa yupo likizo, hivyo kesi hiyo itatajwa kwa hakimu mwingine.
Soma: Kesi ya Dkt. Slaa imeahirishwa mpaka Februari 18, 2025
Vilevile, wakati kesi hiyo inaitwa kwa ajili ya kutajwa mahakamani hapo, tayari Mkurugenzi wa Mashtaka nchini Tanzania amewasilisha kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufani kupinga uamuzi uliotolewa Mahakama Kuu Masjala Ndogo ya Dar es Salaam, ambao ulielekeza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushughulikia suala la dhamana ya mwanasiasa huyo pamoja na mambo mengine.
Chanzo: Mwananchi