mwanamwana
JF-Expert Member
- Aug 1, 2011
- 1,309
- 4,798
MWANASIASA mkongwe na Katibu Mkuu wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa amesema anamuunga mkono Mwenyekiti Chadema, Freeman Mbowe kuhusu uamuzi wa kutangaza kushiriki katika chaguzi zijazo hata kama Serikali haitakuwa tayari kuwapatia Watanzania Katiba mpya.
Akizungumza na MwanaHALISI Online leo Jumatatu, Dk. Slaa amesema historia inaonesha kuwa si mara ya kwanza kudai katiba mpya na kushiriki uchaguzi ambao uliwawezesha kuambulia ushindi katika maeneo machache.
“Chadema imefanya utafiti na kuona angalau hatutamuachia bucha zima fisi, maana yake kama ukimuachia nyama yako italiwa hadi mifupa ila ukishiriki angalau mifupa yako utailinda kuna kitu utaambulia. Tumeona mwaka 2019 CCM ilichukua yote, leo Tanzania nzima inapata hasara, 2020 tumejitoa dakika za mwisho sasa tunaona hela zetu bado watazipiga na wataendelea kwa sababu hatuna wawakilishi. Hivyo lazima tufanye utafiti badala ya maneno ya kisiasa.
“Ukiuliza watu wa mitaani watakuambia tunataka katiba kwanza lakini katiba yenyewe hawaijui, watu hao hao ukiwaita kwenye maandamano hawatokei, sasa utafanya nini? Ushauri wangu wakati tunapoendelea kudai katiba, tuendelee na uchaguzi, kwa sababu kuna vyama vingi vya siasa ambavyo havina ajenda ya Katiba mpya kwenye uchaguzi jambo ambalo vinatufanya tuone vipo kumuunga mkono Rais Samia,” amesema.
Chanzo: Mwanahalisi