Dkt. Slaa: Rais unapoajiri watu wako hatutaki uajiri machawa wanaotumia kodi zetu

Dkt. Slaa: Rais unapoajiri watu wako hatutaki uajiri machawa wanaotumia kodi zetu

Rare Sapphire

JF-Expert Member
Joined
Jul 24, 2021
Posts
590
Reaction score
1,648
Dkt. Slaa akiwa anazungumza katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika leo Julai 12, 2023 asema, Rais anapoajiri watu wake hatutaki uaajiri machawa ambao wanatumia kodi zetu.

Akiongeza kuwa kila siku Rais unatupandishia Tozo kwenye simu, bei ya vyakula na kila kitu na kwenda kulipa machawa wake.

Na kwamba tulimpa kazi Rais Samia kikatiba ili atupatie watu wa kuhudumia taifa hili kwa mujibu wa ibara ya 8 ya katiba ya Tanzania.

Pia soma: Mkutano wa Dkt. Slaa, Askofu Mwamakula, Wakili Mwabukusi na Madeleka
 
Slaa tapeli tu kweli Magu alikua Simba ya yuda hakuna nyau aliongea sijui mama anafeli wapi hawa machekibobu tangu wafutiwe kesi wanaongea sana
 
WILBROAD SLAA ANAPIGA PIGA KELELE AKIDHANI ATAWEZA KUAMBULIA TEUZI,TEUZI HAKUNA UTAPIGA KELELE LAKINI MWISHOWE UTATULIA TU,KELELE ZA CHURA HAZIMZUII ........!
 
Kwahiyo sasa si mkataba ...ila anayeshambuliwa ni Rais personal?
Huu ujinga wako umeurithi wapi?

Kwani aliyeenda uarabuni kuhongwa alikuwa nani? na aliyejisifia ana machawa wa kumlinda alikuwa nani?

Umegeuka debe tupu.
 
Zamani ulipokuwa ukileta story zako za operation za kijeshi nilizani ni mtu mwenye IQ kubwa kumbe daah...
Kichwani hamna kitu.
Ulikuwa una copy na ku-paste
Alikuambia ana hitaji heshima yako. Punguza shobo
 
Back
Top Bottom