Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 2,060
- 5,648
Mwanasiasa mkongwe na aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dkt. Wilbrod Slaa, ametoa ufafanuzi kuhusu kauli ya No Reform, No Election, akisema kuwa si msimamo wa CHADEMA kususia uchaguzi bali kuzuia uchaguzi, na ni wananchi wenyewe ndio watakaoongoza zoezi hilo iwapo hakutakuwa na mabadiliko ya msingi katika sheria za uchaguzi.
Akizungumza kupitia jukwaa la Kumekucha la mtandao wa Clubhouse, Dkt. Slaa amesema kuwa tafsiri ya mwandishi wa habari mwandamizi, Ansbert Ngurumo kuhusu msimamo wa CHADEMA inaweza kuwa na upotoshaji kwa sababu ya ukosefu wa uelewa wa kina juu ya hoja hiyo.
"Taarifa ya Ansbert ikiachiwa ilivyo inapeleka ujumbe wenye shida. Huenda hajaelewa vizuri maana ya No Reform, No Election, na ikiachwa hivyo itakuwa ni upotoshaji. Kuna watu ambao hawana chanzo kingine cha taarifa, wanategemea mitandao, kwa hiyo ukiwapelekea hiyo worries anayoitaja Ansbert kwa sababu tu hajafanya utafiti, itakuwa siyo vizuri," amesema Dkt. Slaa.
Ameeleza kuwa msingi wa kauli ya No Reform, No Election unatokana na mazingira halisi ya uchaguzi nchini, hasa baada ya uchaguzi wa Serikali za Mitaa uliofanyika miezi michache iliyopita, ambao alidai ulikumbwa na dosari nyingi.
"Tujikumbushe kwamba ni miezi mitatu tu tumetoka kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa, na kwa uchafuzi tuliouona, ni mjinga tu anaweza kukubali kushiriki uchaguzi mwingine kabla ya mabadiliko ya msingi katika sheria za uchaguzi. Wenzetu wanapotosha kwa kusema kuwa marekebisho ya sheria yalifanyika mwaka jana, lakini ni wale tu ambao hawajasoma yale marekebisho ndio wanaweza kusema sheria zetu zimeboreshwa," amesema.
Soma, Pia: Lissu: Mabadiliko yakikubaliwa, Uchaguzi utaahirishwa na Bunge litarudishwa hata kama lilivunjwa
Dkt. Slaa alisisitiza kuwa Ibara ya 8 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa mamlaka yote kwa wananchi, hivyo wao ndio wenye uamuzi wa mwisho kuhusu uchaguzi.
"Kwa mara ya kwanza katika historia ya Tanzania, kupitia sheria zilizorekebishwa, wananchi ndio watakaosema No Reform, No Election, siyo CHADEMA inasusia au haitashiriki. Wananchi wenyewe ndio watakaozuia uchaguzi. Hii ni haki yao kwa mujibu wa Ibara ya 8 ya Katiba, inayoeleza kuwa mamlaka yote yatatoka kwa wananchi," amesema.