Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mheshimiwa Dkt. Stergomena Tax (Mb) tarehe 30 Juni 2024 ameungana na Waumini wengine kushiriki Misa ya Jumapili katika Parokia ya Mtakatifu Kizito, Kabila Jimbo la Magu, Mkoani Mwanza.
Katika ibada hiyo, Mheshimiwa Waziri Stergomena Tax, aliungana na Waumini wa Parokia hiyo, Wageni Waalikwa na Viongozi wa Halmashauri ya Wilaya Magu, kushiriki Harambee ya Ujenzi wa nyumba ya Mapadri Kanisani hapo.
Akitoa salamu, Dkt. Tax amekumbusha kuwa Taasisi za dini ni muhimu sana kushirikiana na Serikali katika Nyanja mbaili mbali ili kuleta maendeleo katika jamii, na kudumisha amani na mshikamano, na kuwawaomba Viongozi wa dini na Waumini kuendelea kushirikiana na Serikali na kuliombea Taifa letu Tanzania na Viongozi wake. Aliwahakikishia kuwa Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inawajali kama ambavyo wanaendekea kushuhudia.
Aidha, amewakumbusha Wananchi kujitokeza kwenye zoezi la uboreshaji taarifa za mpiga Kura katika Daftari la wapiga kura ambalo limefunguliwa tarehe 1, Julai 2024 nchi nzima, ili watumie haki yao ya ki Katiba na kupata fursa ya kuchagua Viongozi wanaowataka wakati wa Uchaguzi.