Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 48,475
- 70,102
Nimeona clip moja ya Sheikh mwanaharakati, Dr Sulle akisema watu wengi hawajui au wanapotosha hayati Rais Mwinyi kuitwa Mzee Ruksa.
Akitoa historia fupi Dr Sulle anasema mwaka 1993 kulitokea vurugu kubwa Dar es Salaam baada ya msichana mmoja wa Kiislamu aliyetumwa kununua nyama kukosea na kwenda kununua kitimoto katika bucha mojawapo la Nguruwe lilikuwepo Tandale.
Baada ya habari hiyo kusambaa anasema walifanya vurugu kubwa iliyosababisha uharibifu mkubwa wa mali pamoja na kutishia amani. Ndipo hayati Rais Mwinyi alipohutubia taifa katika kutuliza hali kwa hekima na katika kuwafanya Wakristo na Waislamu waishi kwa pamoja kwa upendo baada ya kutoa nasaha nyingi akatamka katika hotuba yake nchi hii haina dini, kila mtu mwenye kutaka chake na ale, mwenye kutaka jongoo ale ruksa, mwenye kutaka panya ale ruksa, na hapo ndipo neno ruksa lilianzia.
Pamoja na hilo, Dr Sulle anasema pia Mwinyi ndiye baba wa mageuzi wa uchumi na siasa wa taifa hili na hakuna Rais aliyelitendea haki taifa hili kumzidi Mwinyi.
Mwanahistoria Mohamed Said ni kweli hayati Rais mwenye kuitwa Mzee Ruksa sio kutokana na yeye kuleta uhuru wa biashara na siasa nchini bali hilo neno liliibuka kutokana na vurugu zilizohusisha nguruwe Tandale?