Mkalukungone mwamba
JF-Expert Member
- Aug 29, 2022
- 862
- 1,755
Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini, Dkt.Tulia Ackson ameshiriki zoezi la kupiga kura na kumchagua kiongozi amtakaye huku akisisitiza wananchi kujitokeza kwa wingi kupiga kura na kuwa watulivu baada ya kutangazwa matokeo.
Dkt. Tulia ametoa rai hiyo baada ya kushiriki uchaguzi katika kituo cha Uzunguni A (Shule ya Msingi Umoja, Kata ya Sisimba jijini Mbeya).
Soma Pia: Yanayojiri kuelekea uchaguzi Serikali za Mitaa mkoa wa Mbeya
Katika hatua nyingine Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Bw.Juma Homera amesema katika mkoa wake hali ya usalama ni shwari kutokana na Jeshi la Polisi lilivyojipanga vema kwa kuhakikisha raia na mali zao wako salama.